RAIS SAMIA ARIDHIA WATUMISHI WALIOTUMBULIWA VYETI FEKI KUREJESHEWA MICHANGO YAO

RAIS SAMIA ARIDHIA WATUMISHI WALIOTUMBULIWA VYETI FEKI KUREJESHEWA MICHANGO YAO

Na Barnabas Kisengi Dodoma RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Mhe SAMIA SULUH HASSAN ameridhia Watumishi wote wasiopungua 14,516 walioondolewa kazini kwa kughushi vyeti warejeshewe michango yao tu waliyokatwa kwenye mishahara na kuwasilishwa kwenye Mifuko ya Hifadhi ya jamii.Kufuatia uchambuzi uliofanyika baada ya kuondolewa kwenye Utumishi wa Umma watumishi hao wamekuwa wakitumia njia mbalimbali,

Na Barnabas Kisengi Dodoma


RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Mhe SAMIA SULUH HASSAN ameridhia Watumishi wote wasiopungua 14,516 walioondolewa kazini kwa kughushi vyeti warejeshewe michango yao tu waliyokatwa kwenye mishahara na kuwasilishwa kwenye Mifuko ya Hifadhi ya jamii.
Kufuatia uchambuzi uliofanyika baada ya kuondolewa kwenye Utumishi wa Umma watumishi hao wamekuwa wakitumia njia mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kutumia Vyama vya Wafanyakazi kuomba walipwe mafao kutoka kwenye mifuko hiyo.


Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,Vijana,Ajira, na Wenye Ulemavu) Prof.Joyce Ndalichako amesema hayo wakati Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma kufuatia maelekezo hayo ,amesema kuwa Mifuko ya Hifadhi ya jamii ya PSSSF na NSSF itarejesha michango ya Wafanyakazi iliyowasilishwa kwenye Mifuko hiyo bila kuhusisha michango ya mwajiri.


“Kama mnavyokumbuka katika kipindi cha kuanzia Mwezi Oktoba, 2016 hadi April,2017 ,Serikali iliendesha zoezi maalum la uhakiki wa vyeti kwa kushirikiana na Baraza la Mitihani la Taifa ( NACTE),kufuatia Uhakiki huo ,watumishi wasiopungua 14,516 walibainika kuwa na vyeti vya kughushi na walioondolewa katika utumishi wa Umma,”amesema Prof Ndalichako
 “Wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani tarehe 01 Mei ,2022 ,Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) kupitia risala yao,waliwasilisha ombi kwa Mheshimiwa Rais aangalie namna ya kuwafuta Jasho lao ambapo Rais katika hotuba yake kwenye siku hiyo alielekeza kufanyika kwa uchambuzi ili kuona namna gani ambavyo Serikali inaweza kuhitimisha suala hilo,”amesma Prof.Ndalichako.


Waziri Prof.Ndalichako amewataka waajiri kuwajibika kuwasilisha kwenye Mifuko Hati za Ridhaa pamoja na nyaraka nyingine zinazohusu ulipaji wa mafao kwa kuzingatia taratibu na miongozo ya Mifuko husika.
“Mara baada ya Mifuko Kupokea nyaraka kutoka kwa aliyekuwa Mwajiri,malipo yatafanyika kupitia akauti za benki na marejesho ya michango ya Watumishi hao, yataanza kufanyika kuanzia tarehe 1 Novemba, 2022,”ameeleza Prof.Ndalichako.

Waziri wa nchi ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Jenista Mhagama amesema kuwa hatua hii iliyochukuliwa na Mhe.Rais ni ya huruma na upendo mkubwa kwa Watumishi hao.


Mhagama akawataka Waajiri wote nchini kutoa ushirikiano kwa Watumishi wakati wa kutekeleza zoezi hilo na kujiepusha na vitendo vya rushwa ambavyo vinaweza kuchelewesha na kupelekea kuharibu dhamira njema ya Mhe.Rais.
“Niwaagize Waajiri wote kutekeleza zoezi hili kwa kuzingatia misingi ya utawala bora ikiwemo kuepukana na vitendo vyovyote vitakavyoashiria uwepo wa Rushwa katika kutimiza adhma hii ya a,” Amesisitiza Wazazi Mhagama
Waziri Mhagama ametoa wito kwa TAKUKURU kutumia kila mbinu kuhakikisha wanazuia vitendo vyote vya Rushwa pindi zitakapojitokeza.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »