MATUMIZI YA INTANETI YAMEONGEZEKA KWA ASILIMIA 4.2 KUTOKA MILIONI 29,858,759 HADI 31,122,163.

MATUMIZI YA INTANETI YAMEONGEZEKA KWA ASILIMIA 4.2 KUTOKA MILIONI 29,858,759 HADI 31,122,163.

Na Moreen Rojas-Dodoma Takwimu za sasa zinaonesha matumuzi ya intaneti yameongezeka kwa asilimia 4.2 kutoka milioni 29,858,759 mwaka 2021 hadi kufukia 31,122,163 mwezi septemba 2022.Hayo yameelezwa na Dkt.Jabir Bakari Mkurugenzi Mkuu (TCRA) wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu taarifa ya utendaji wa majukumu kwa mwaka 2021/22 na mpango kazi 2022/23. Amesema kuwa

Na Moreen Rojas-Dodoma


Takwimu za sasa zinaonesha matumuzi ya intaneti yameongezeka kwa asilimia 4.2 kutoka milioni 29,858,759 mwaka 2021 hadi kufukia 31,122,163 mwezi septemba 2022.
Hayo yameelezwa na Dkt.Jabir Bakari Mkurugenzi Mkuu (TCRA) wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu taarifa ya utendaji wa majukumu kwa mwaka 2021/22 na mpango kazi 2022/23.


Amesema kuwa mwelekeo wa ongezeko la watumiaji wa intaneti inaonyesha kwamba kulikuwa na ukuaji wa takribani asilimia 17 kila mwaka,katika kipindi cha miaka 5 ambapo mwaka 2017 kulikuwa na watumiaji milioni 16,106,636 na mwishoni mwa mwaka 2021 waliongezeka kufikia milioni 29,103,482.
“Ongezeko la matumizi ya intaneti limechangiwa pia na matumizi ya kiswahili,maudhui ya kiswahili kwenye intaneti yameongezeka kwa kasi na program tumizi(application) kwa lugha ya kiswahili zimeongezeka pia kumekuwa na juhudi za kuendeleza na kueneza matumizi ya kiswahili kimataifa” Amesema Dkt.Jabir.


Aidha ameongeza kuwa ripoti hii ya utendaji wa sekta ya mawasiliano nchini zinabainisha mitandao mitano(5) ya kijamii inayotumiwa zaidi ,hivyo kuongoza kwa kiwango kikubwa cha data iliyotumika kwa kipimo cha GB,ambapo mtandao wa kijamii wa Facebook uliongoza kwa kurekodi ( GB Bilioni 2.59),ukifuatiwa na YouTube wenye (GB Bilioni 1.91), kisha WhatsApp uliokuwa na (Bilioni 1.58), na Tik Tok ukiwa na ( GB Milioni 999)ikifuatiwa na mitandao mingine.

Amesema kuwa idadi ya miamala imeongezeka kutoka Bil.349,952,830 hadi miamala Bil.366,178,409 septemba 2022,aidha akaunti za pesa kwa simu zimeongezeka kwa asilimia 1.5 katika miezi tisa iliyopita kuanzia januari hadi septemba 2022,wakati miamala ikiongezeka kwa asilimia 2.
Kwa upande wa takwimu za utangazaji zinaonyesha kwamba visimbuzi 3,326,845 vilikuwa hewani hadi septemba 2022,kati ya hivyo 1,656,460 ni vya dijitali kwa mfumo wa televisheni wa utangazaji wa mitambo ya ardhini (DTT) kulinganisha na 1,670,385 kwa mfumo wa televisheni kwa satelaiti.


Dar es Salaam inaongoza kwa kuwa na visimbuzi ( 218,007) ambapo mikoa yenye visimbuzi vichache ni Songwe ( 1,568) ukifuatiwa na katavi (16,990).
Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali Ndg.Gerson Msigwa ampongeza Dkt.Jabir kwa kuweza kutoka ufafanuzi mzuri kwa wananchi kuhusu taasisi hiyo na kusema kuwa kwa uwekezaji ambao umefanywa na Serikali kupitia ( TCRA) huwezi kufanya uhalifu usikamatwe.
” Nawasihi vijana kufanya kazi kwa kufata taratibu za uandishi wa habari ili kuweza kuepuka vikwazo vidogovidogo na badala yake kutumia fursa zilizopo kwenye App mbalimbali ili kuweza kukua kiuchumi”Amesisitiza Ndg.Msigwa.


TCRA inaendelea kusimamia Sekta ya mawasiliano ikiwa ni pamoja na kushirikiana na wadau mbalimbali katika ngazi ya kitaifa,kikanda na kimataifa ili kuhakikisha sekta ya mawasiliano inatoa mchango katika maendeleo ya nchi na kuwa kichocheo cha ukuaji wa uchumi wa kidijitali na uchumi wa buluu.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »