WIZARA YA FEDHA YAANDAA WIKI YA HUDUMA ZA FEDHA KITAIFA

Na, Wellu Mtaki, Dodoma Wizara ya fedha na mipango imeandaa wiki ya huduma za fedha kitaifa ambayo lengo lake ni kutoa Elimu kwa wananchi ili kujenga uelewa na weledi katika matumizi sahihi ya fedha lengo likiwa ni kukuza  uchumi na kuondoa umasikini. Kauli hiyo Imetolewa leo November 15  mwaka huu jijini dodoma na kamishina wa

Na, Wellu Mtaki, Dodoma

Wizara ya fedha na mipango imeandaa wiki ya huduma za fedha kitaifa ambayo lengo lake ni kutoa Elimu kwa wananchi ili kujenga uelewa na weledi katika matumizi sahihi ya fedha lengo likiwa ni kukuza  uchumi na kuondoa umasikini.


Kauli hiyo Imetolewa leo November 15  mwaka huu jijini dodoma na kamishina wa Wizara ya Fedha na Mipango Charles Mwamwaja alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wiki ya huduma ya fedha kitaifa ambayo mwaka huu yatafanyika jijini mwanza kuazia November 21 hadi 26 mwaka 2022.

Amesema kuwa elimu ya fedha ni jambo muhimu sana kwa umma kwa kuwa itawezesha kusimamia vinzuri lasilimali fedha, kuhifadhi akiba , Namna ya kukopa pamoja na pamoja na kulinda kipato chake.

Aidha amesema kuwa lengo lingine la wiki ya huduma ya fedha kwa mwananchi ni Kuwezesha wajasiliamali wadogo kuongeza ujuzi na matumizi sahihi ya huduma ya fedha katika kukuza biashara zao.


Mwamwaja ameongeza kuwa wiki ya huduma ya fedha inalenga kuwafikia wadau mbalimbali wakiwemo Watumishi wa Umma, wanafunzi, wakufunzi, wanawake, vijana, watu wenye maitaji maalumu, wajasiliamali wadogo na wakati,asasi za kiraia, wahariri, waandishi wa vyombo vya habari, watoa huduma za fedha, watoto na umma kwa ujumla.


Pia ametoa wito kwa wanainchi wa jiji la mwanza na mikoa jirani kujitokeza kwa wingi katika maazimisho hayo ambayo kea mwaka huu kaulimbiu yake inasema Elimu ya Fedha kwa Maendeleo ya watu.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »