ADEM YADAHILI WALIMU 1,839 MAFUNZO YA UDHIBITI UBORA NA USIMAMIZI ELIMU

ADEM YADAHILI WALIMU 1,839 MAFUNZO YA UDHIBITI UBORA NA USIMAMIZI ELIMU

Na Moreen Rojas,Dodoma. Wakala wa maendeleo ya Uongozi wa elimu (ADEM) imedhahili walimu 1,839 katika mafunzo ya stashahada ya uongozi na usimamizi wa elimu DEMA na stashahada ya udhibiti ubora wa shule DSQA ili kuwapa ujuzi na maarifa walimu katika usimamizi,ufuatiliaji na tathimini katika elimu. Hayo yameelezwa na mtendaji mkuu wa wakala (ADEM) Dkt.Siston Mgullah

Na Moreen Rojas,Dodoma.


Wakala wa maendeleo ya Uongozi wa elimu (ADEM) imedhahili walimu 1,839 katika mafunzo ya stashahada ya uongozi na usimamizi wa elimu DEMA na stashahada ya udhibiti ubora wa shule DSQA ili kuwapa ujuzi na maarifa walimu katika usimamizi,ufuatiliaji na tathimini katika elimu.


Hayo yameelezwa na mtendaji mkuu wa wakala (ADEM) Dkt.Siston Mgullah wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za wakala hiyo na mwelekeo wa utekelezaji kwa mwaka wa fedha wa 2022/23.
Dkt.Mullah amesema katika mwaka huu wa fedha 2022/23 wakala hiyo imejipanga kudahili walimu 2343 katika kozi za CELMA,DEMA na DSQA kuandaa mwongozo wa utawala bora kwa viongozi wa serikali za mitaa.
“Wakala imejipanga kutoa mafunzo ya uongozi na usimamizi wa shule kwa walimu wakuu wapatao 17,000 kutoa mafunzo ya utawala bora kwa wasimamizi wa elimu katika mamlaka na serikali za mitaa” Amesema Dkt.Mgullah.


Mtendaji huyo amesema kuwa wakala hiyo imetoa mafunzo ya muda mfupi kuhusu uthibiti ubora wa shule wa ndani kwa walimu 7,612 ili kuwajengea uwezo wa kusimamia ufundishaji na ujifunzaji katika shule wanazosimamia.


Dkt.Mgullah ameongeza kuwa wakala pia umeendesha mafunzo ya muda mfupi kwa walimu wakuu na waratibu wa taaluma 147 kutoka katika shule za msingi na sekondari Zanzibar chini ya mradi wa Mwanamke Intiative Foundation (MIF).


Pia wakala umeendesha mafunzo ya kamati za shule kwa washiriki 126 katika mkoa wa Songwe ili kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji katika shule na umeandaa mtaala wa shahada ya menejimenti ya uthibiti ubora wa elimu ili kuimarisha usimamizi na utoaji wa elimu bora katika ngazi zote za elimu.
“Tumefanya tafiti sita na tumewasilisha kwa wadau mbalimbali wa elimu ili kubaini mapungufu na kuandaa mafunzo wezeshi kwa wahusika”
“Katika kipindi cha mwaka 2020/2021 wakala umefanya tafiti mbalimbali zikiwemo za tathimini ya matokeo ya mafunzo ya KKK kwa walimu na darasa la III na IV yaliyofanyika Tanzania bara,utekelezaji na uthibiti ubora wa shule na utoaji wa mrejesho kwa walimu ili kuboresha ufundishaji na ujifunzaji katika shule za msingi ” Dkt. Mgullah.


Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa serikali na Mkurugenzi mkuu wa idara ya habari maelezo Gerson Msigwa amesema kuwa serikali imeweka fedha nyingi kwenye sekta ya elimu nchi nzima ambapo kwa mwaka wa fedha 2022/23 sekta ya elimu imetengewa shilingi trilioni 5.8 chuo hiki ni moja ya juhudi za serikali za kusimamia ubora wa elimu.


Pia Msigwa ametoa wito kwa waajiri kuwaruhusu viongozi wa taasisi za elimu kwenda kusoma ADEM kwani watakuwa tofauti na mabadiliko yataonekana ikiwa ni pamoja na kuongeza ubunifu na usanifu kwa kukuza sekta ya elimu nchini.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »