KATIBU MKUU CCM TAIFA AMEWATAKA WAJUMBE WA UCHAGUZI WA MIKOA KUCHAGUA VIONGOZI WAADILIFU.

KATIBU MKUU CCM TAIFA AMEWATAKA WAJUMBE WA UCHAGUZI WA MIKOA KUCHAGUA VIONGOZI WAADILIFU.

Na Moreen Rojas, Dodoma. Katibu Mkuu CCM Ndg.Daniel Chongolo amewataka wajumbe wa uchaguzi wa mikoa kuchagua viongozi waadilifu. Chongolo ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Covention jijini Dodoma. Amesema kuwa wameamua kusimamisha uchaguzi wa vijana mkoa wa Simiyu kutokana na rushwa,kusimamisha uchaguzi wa nafasi ya mjumbe Mbeya kwa

Na Moreen Rojas, Dodoma.

Katibu Mkuu CCM Ndg.Daniel Chongolo amewataka wajumbe wa uchaguzi wa mikoa kuchagua viongozi waadilifu.

Chongolo ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Covention jijini Dodoma.

Amesema kuwa wameamua kusimamisha uchaguzi wa vijana mkoa wa Simiyu kutokana na rushwa,kusimamisha uchaguzi wa nafasi ya mjumbe Mbeya kwa tuhuma za rushwa,kusimamisha uchaguzi wa mjumbe wa halmashauri kuu kutokana na tuhuma za rushwa.

“Uchaguzi unaendelea vizuri sana,tutahakikisha haki inatendeka pamoja na kufanya uchunguzi wa kina kama kuna changamoto yoyote tutasitisha kupisha uchunguzi kama hakuna basi tutaendelea” Amesema Chongolo.

Aidha amesema uchaguzi uliofanyika jana mkoa wa magharibi Zanzibar kueleza tukio la mmoja wa wanachama kuchukua sanduku la kupigia kura na kuondoka nalo tukio hilo linafanyiwa uchunguzi na ikibainika kwenda kinyume na taratibu hatua kali zitachukuliwa na mamlaka husika.

“Mtu yoyote atakayetumia ujanjaujanja tutashughulika nae ipasavyo,tuache ujanja wa kutumia majina ya viongozi wetu kwa kutumia hila,uzushi na ujanjaujanja”

Ameongeza kuwa watu watakaotumia njia za rushwa na mbinu za ujanjaujanja hatua zitakazochukuliwa ni kuwaondoa kugombea kwa kushirikiana na mamlaka husika.

Kwa Mikoa ambayo inatuhumiwa na vitendo vya rushwa na udanganyifu chama kimeamua kusimamisha uchaguzi kwa maeneo hayo ili kupisha uchunguzi,na matumaini yetu wote uchunguzi utakamilika mara moja.

Amesema kwa maeneo ambayo hayana tuhuma hizo uchaguzi unaendelea kama kawaida na kuwataka wajumbe kuwa wazalendo na waadilifu kwa kukataa vitendo vya rushwa.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »