WAZIRI KAIRUKI AMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUCHAGIZA MAENDELEO SEKTA YA ELIMU

WAZIRI KAIRUKI AMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUCHAGIZA MAENDELEO SEKTA YA ELIMU

Angela Msimbira, MANYARA Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Angellah Kairuki amemshukuru Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kuchagiza maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwenye sekta ya elimu.Waziri Kairuki ameyasema hayo leo Novemba 22, mwaka huu alipokuwa akizungumza na wananchi

Angela Msimbira, MANYARA


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Angellah Kairuki amemshukuru Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kuchagiza maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwenye sekta ya elimu.
Waziri Kairuki ameyasema hayo leo Novemba 22, mwaka huu alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Manyara kwenye mkutano wa hadhara katika ziara ya kikazi ya Rais Samia.

Amesema  katika mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali  kupitia fedha za UVIKO- 19 ilielekeza Sh.bilioni 300  kwa ajili ya kujenga madarasa 12,000 katika shule za Sekondari na madarasa 3000 kwa shule shikizi.
Waziri Kairuki ameeleza kuwa kupitia fedha hizo  watoto 907,000  wameingia  kidato cha kwanza kwa mwaka 2022 na hakukuwa na mtoto aliyebaki nyumbani kusubiri awamu ya pili ya kuchaguliwa.


Amesema kuwa kupitia fedha hizo za UVIKO-19 Mkoa wa Manyara ulipata zaidi ya sh. bilioni 5.5 kwa ajili  ya madarasa ya shule za sekondari, pia wamepata sh. bilioni 2 3 kwa ajili ya kujenga madarasa ya shule shikizi.

Aidha, Waziri Kairuki amesema  Serikali imetoa kiasi cha sh. bilioni 160  kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 8000 nchi nzima na kwa upande wa Mkoa wa Manyara  umepata sh.bilioni 1.54 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 77  ili watoto wanaoingia kidato cha kwanza  2023.
Vile vile, Waziri Kairuki ameeleza kuwa kipitia mradi wa kuimarisha elimu ya sekondari nchini (Sequip)  Sh.trilioni 1.2 zimetolewa ambapo  mpaka sasa sh.  bilioni 143.47 zimetumika katika ujenzi wa  shule 2.32  katika mwaka wa fedha 2021/22.


Amesema katika mwaka wa fedha 2022/23 Serikali itajenga shule 184 katika Halmashauri zote ambapo kila shule itagharimu sh.milioni 600 lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa hakuna kata ambayo itakuwa haina shule ya Sekondari.
Aidha, amesema kuwa kwa miaka mitano Serikali itajenga shule 1026 kupitia mradi wa Sequip na kupitia mradi wa kuboresha elimu ya awali na msingi itaboresha madarasa zaidi ya 9000 yenye thamani ya sh. bilioni 250.9.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »