Na; Emesto Eliudy, Dar Es Salaam Serikali kupitia Wizara ya elimu nchini, imeshauriwa kuandaa mitaala rafiki Kwa ajili ya masomo Kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari ili kuwajengea uwezo mkubwa na uelewa mpana wa elimu wanafunzi hao. Ushauri huo umetolewa jijini Dar Es Salam na Mchungaji wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la
Na; Emesto Eliudy, Dar Es Salaam
Serikali kupitia Wizara ya elimu nchini, imeshauriwa kuandaa mitaala rafiki Kwa ajili ya masomo Kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari ili kuwajengea uwezo mkubwa na uelewa mpana wa elimu wanafunzi hao.
Ushauri huo umetolewa jijini Dar Es Salam na Mchungaji wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Mashariki Ushirika wa Tabata, Mch. Emmanuel Mahembo baada ya kumaliza ibada ya kuombea Msimu mpya kwa wanafunzi wanaorudi shuleni ambapo amesema Kuwa Serikali Ina wajibu wa kuboresha miundombinu ya shule ili wanafunzi wasome katika mazingira rafiki na kuwaongezea ufaulu wanafunzi hao.

Akizungumza Kwa niaba ya wazazi, Atuganile Mjwanga, amesema kuwa wazazi wamekuwa na majukumu mengi kiasi ambacho wanasahau kuwaombea watoto ambao wapo kwenye shule mbalimbali hivyo amewataka wazazi kutenga muda wa kuwafuatilia watoto wao.

Kwa upande wake Daniel Hamphrey ambaye ni mwanafunzi wa kidato Cha pili amelishukuru Kanisa Hilo Kwa kuona umuhimu wa kuwaombea huku akiwasihi wanafunzi kumtegemea Mungu Zaidi katika masomo yao.

Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *