BILIONI 6 KUBORESHA HOSPITALI YA MIREMBE

BILIONI 6 KUBORESHA HOSPITALI YA MIREMBE

Na Barnabas Kisengi Dodoma Serikali kupitia wizara ya Afya imetumia zaidi ya Tsh Bilioni 6 kuboresha miundombinu ya hospital ya Taifa ya Afya ya Mirembe Jijini Dodoma. Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya miradi ujenzi na kuongea na watumishi wa hospitali hiyo Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema ujenzi huo umefikia

Na Barnabas Kisengi Dodoma


Serikali kupitia wizara ya Afya imetumia zaidi ya Tsh Bilioni 6 kuboresha miundombinu ya hospital ya Taifa ya Afya ya Mirembe Jijini Dodoma.


Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya miradi ujenzi na kuongea na watumishi wa hospitali hiyo Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema ujenzi huo umefikia hatua za mwisho hivyo itasaidia wananchi kupata huduma za afya ya Akili katika mazingira bora
“Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt SAMIA SULUH HASSAN  imetoa zaidi ya Bilioni 6 katika kuboresha miundombinu pamoja na vifaa tiba katika hospitali hii, sasa ni jukumu lenu watumishi kuboresha na kutoa huduma bora kwa wananchi ikiwemo matumizi ya lugha nzuri”Alisisitiza Dkt. Mollel.


Dkt. Mollel ameiagiza MSD ndani ya miezi miwili kuhakikisha inapeleka vifaa vya upasuaji wa mifupa katika hospitali hiyo ili wananchi waanze kunufaika na huduma hiyo ambayo awali walikua wakiifuata umbali mrefu.
“MSD  leteni vifaa  vya upasuaji dani ya miezi miwili pia mnatakiwa kutoa kibali cha kununua dawa kwa watu binafsi kwa vituo vyote vya kutolea hhuduma za afya nchini ndani ya saa 24 endapo dawa zinahitajika na hazipo MSD ili kuondoa usumbufu unaoweza kuzuilika kwa wananchi”Alisisitiza.


Aidha Dkt. Mollel amewashauri viongozi wa hospitali hiyo kuanza kufikiria namna ya kuongeza huduma nyingine ili kutanunua wigo wa kuwahudumia wananchi wenye uhitaji bila kuathiri huduma maalumu za magonjwa ya afya ya Akili zinazotolewa katika Taasisi hiyo.


Naibu Waziri wa Afya ameagiza hospitali hiyo kupatiwa gari ya kubebea wagonjwa kutokana na unyeti wa huduma katika hospitali hiyo ili kuokoa maisha ya wananchi wanaipata huduma Katika hospital hiyo.


Aidha Dkt. Mollel amewaelekeza Wakuu wa Hospitali zote nchini kuacha tabia ya kuwazuia wagonjwa wa rufaa kutoka kituo kingine chochote bila kujali huduma ya mgonjwa huyo ni wa msamaha au la,hiyo itasaidia kuondoa changamoto kwa wagonjwa ikiwemo vifo vinavyoweza kuzuilika.


Naye,Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kutoka Wizara ya Afya Bi. Deodatha Makani amesema wakati hospitali hiyo inaelekea kuwa taasisi ni muhimu watumishi kujipanga na kuwahuduma wananchi kwa ubora wa juu ili kuendana na hadhi ya kuwa taasisi, huku akiweka wazi kwamba Wizara itaendelea kutatua changamoto zote za watumishi.


Kwa upande Wake Mkurugenzi wa Huduma za Tiba, Wizara ya Afya Prof. Paschal Ruggajo amesema wakati Serikali inaelekea kutekeleza Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote lazima viongozi na watumishi wajipange vizuri katika utendaji wao ikiwemo kuboresha na kutoa huduma bora kwa wananchi hasa matumizi ya lugha nzuri na muda mfupi wa kuwahudumia wananchi wanaofika kupata huduma

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »