NAIBU WAZIRI KUNDO ASISITIZA UHAKIKI WA USAHIHI YA ANUANI ZA MAKAZI

NAIBU WAZIRI KUNDO ASISITIZA UHAKIKI WA USAHIHI YA ANUANI ZA MAKAZI

Na Barnabas Kisengi Malinyi Morogoro Serikali imesisitiza wananchi na taasisi kuhakiki taarifa zao za Anwani za Makazi nchini  kuwa taarifa hizo niza msingi katika kutoa na kupokea huduma kwa kuhakikisha kuwa mawasiliano yote yakiwemo ya barua yanatumia Anwani za Makazi, fomu zote za kutolea na kupokelea huduma na Mifumo ya Huduma ya Kielektroniki inajumuisha kipengele

Na Barnabas Kisengi Malinyi Morogoro


Serikali imesisitiza wananchi na taasisi kuhakiki taarifa zao za Anwani za Makazi nchini  kuwa taarifa hizo niza msingi katika kutoa na kupokea huduma kwa kuhakikisha kuwa mawasiliano yote yakiwemo ya barua yanatumia Anwani za Makazi, fomu zote za kutolea na kupokelea huduma na Mifumo ya Huduma ya Kielektroniki inajumuisha kipengele cha Anwani za Makazi ikiwa ni pamoja na utambulisho wa aina yoyote. 


 Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew Amesema hayo akiwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya mawasiliano, ubora na upatikanaji wa huduma za mawasiliano, usikivu wa redio TBC na uhakiki wa Anwani za Makazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi  mkoani Morogoro 
“Baada ya Operesheni ya Anwani za Makazi mfumo upo tayari kutumika. Aidha, kabla ya kutumia wananchi na taasisi tunapaswa kuhakiki taarifa zetu za Anwani za Makazi zilizokusanywa na kuanza kutumia mfumo huu katika shughuli zote za kijamii na kiuchumi ili tupate manufaa tarajiwa”. Amesisitiza Naibu Waziri Kundo.


Aidha Naibu Waziri amebainisha kuwa uhakiki wa taarifa za Anwani za Makazi unategemea eneo ambalo taasisi ama mwananchi alipo ama anapoishi. Pia, eneo linaweza kuwa lenye barabara ama mtaa au lisilo na barabara ama mtaa. Ambapo, kwa maeneo yenye barabara ama mitaa, taasisi ama mwananchi anapaswa kujua nambari ya nyumba, jina la barabara na postikodi ambayo ni nambari maalumu ya kata.
Vilevile katika maeneo ambayo hayana barabara ama mitaa, taasisi ama mwananchi anapaswa kujua nambari ya nyumba, jina la kitongoji, jina la kijiji na postikodi. 


Naibu waziri Amefafanua kuwa ili kufanikisha utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa na Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, viongozi na watendaji wanaombwa kuendelea kutoa elimu kwa umma hususan kuwafahamisha na kuwaelewesha Anwani zao za Makazi sambamba na namna bora ya kutumia Mfumo wa Kidigitali wa Anwani za Makazi (NaPA). 


Aidha Naibu Waziri Mhandisi kondo  amebainisha kuwa ni vyema uratibu wa utekelezaji na matumizi ya mfumo uimarishwe katika ngazi ya halmashauri. Vilevile, wakusanya taarifa waliotumika katika kukusanya taarifa wakati wa operesheni ni vyema waendelee kutambuliwa na kutumika katika kusaidia wananchi wanapopata changamoto za anwani katika maeneo yao.
“Utekelezaji wa Mfumo wa Anwani za Makazi ni endelevu kwa sababu makazi yanaendelea kuongezeka, nyumba zinaendelea kujengwa na watu ama ofisi huendelea kubadilisha makazi ama kuhama.

Hivyo, mnaombwa kuendelea kuweka jitihada za uendelezaji wa mfumo kwa kuweka miundombinu, kukusanya taarifa na kusahihisha taarifa”. Amesisitiza Naibu Waziri Mhe. Mhandisi Kundo.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »