WAZIRI JAFO AHIMIZA UPANDAJI MITI KUHIFADHI MAZINGIRA

WAZIRI JAFO AHIMIZA UPANDAJI MITI KUHIFADHI MAZINGIRA

Na Barnabas Kisengi Dodoma. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira  Dkt. Selemani Jafo amesema ndani ya kipindi cha miaka miwili Tanzania imepiga hatua katika kusukuma mbele ajenda ya mazingira kwa upandaji miti na kutunza Mazingira hapa nchini. Dkt Jafo Amesema hayo January 27, 2023 wakati akizungumza baada ya kuongoza zoezi

Na Barnabas Kisengi Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira  Dkt. Selemani Jafo amesema ndani ya kipindi cha miaka miwili Tanzania imepiga hatua katika kusukuma mbele ajenda ya mazingira kwa upandaji miti na kutunza Mazingira hapa nchini.

Dkt Jafo Amesema hayo January 27, 2023 wakati akizungumza baada ya kuongoza zoezi la upandaji miti katika kituo cha kulea watoto cha Nyumba ya Matumaini kilichopo Miyuji jijini Dodoma na kumtakia heri ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. SAMIA SULUH HASSAN kwa kutimiza umri wa miaka 63.

Aidha Waziri Dkt Jafo amempongeza Rais Dkt. SAMIA SULUH HASSAN kwa kuwa mwanamazingira namba moja nchini na duniani akimtaja kuwa amekuwa akihamasisha wananchi kushiriki shughuli za kuhifadhi mazingira katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

” Desemba 21, 2017 alizindua Kampeni ya Kukijanisha Dodoma katika eneo la Mzakwe jijini Dodoma hivyo katika kumuenzi mabalozi wa mazingira wamefanya kazi nzuri ya kuhamasisha upandaji miti katika maeneo mbalimbali Mkoani Dodoma ili kuhakikisha Dodoma inakuwa ya kijani” amesema Waziri Dkt Jafo.

Dkt. Jafo pia amewashukuru mabalozi wa mazingira na wataalamu kutoka Jiji la Dodoma kwa kuandaa zoezi hilo na kusema kuwa ni la muhimu katika kuhakikisha mazingira yanahifadhiwa kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Waziri  Dkt Jafo amesema kuwa zoezi la upandaji miti limekuwa na mwitikio mkubwa miongoni mwa wanafunzi wa shule, vyuo na jamii kwa ujumla ambapo inashuhudiwa wananchi wakihamasika kupanda miti katika maeneo mbalimbali Mkoani Dodoma.

“Hapa leo tumeadhimisha siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Mhe RAIS Dkt SAMIA SULUH HASSAN  kwa kuendeleza kampeni kabambe ya upandaji miti Tanzania nimefarijika sana kuona wanafunzi wanashiriki kupanda miti hapa na inadhihirisha namna gani nchi yetu imepiga hatua katika swala la mazingira,” amesema Dkt Jafo.

Aidha, Dkt. Jafo ametoa wito kwa wananchi kujiepusha na tabia ya ukataji miti ovyo kwa ajili ya kuni na mkaa na badala yake watumie nishati mbadala ili kuepuka changamoto za athari za mabadiliko ya tabianchi.

Pia, amesema kuwa hivi karibuni Serikali itatoa maelekezo rasmi kwa taasisi mbalimbali kuanza kutumia nishati mbadala kwa ajili ya kupikia na kuachana na matumizi ya mkaa na kuni kama ilivyo hivi sasa.

Kwa upande wake Mwakilisha wa mabalozi wa mazingira Bi. Oliver Nyeriga amesema zoezi la upandaji miti lililofanyika katika kituo hicho mbali ya kusaidia kutunza mazingira lakini pia ni njia mojawapo ya kupunguza utegemezi.

“Hapa leo tumefanya zoezi la upandaji miti ambalo pia linatufanya tuwe wabunifu zaidi kwani miti hii ya matunda ikikua itawasaidia wanaoishi hapa kujipatia kipato kwa kuuza matunda yatakayopatikana hapa,” amesema Bi. Oliver Nyeriga.

Katika zoezi hilo pia waziri Dkt Jafo alipata wasaa wa kulishwa keki katika kituo hicho kuonyesha upendo wa dhati katika siku ya kumbukizi ya sikukuu ya kuzaliwa kwa RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe  Dkt SAMIA SULUH HASSAN kwa kutimiza umri wa miaka 63 tangu azaliawe hivyo watanzania wametakiwa kuendelea kumwombea heri na baraka tele katika utendaji Wake wa majukumu RAIS Wetu Mhe Dkt SAMIA SULUH HASSAN.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »