RC SENYAMULE AMWAPISHA DC MPYA- CHEMBA MHE. GERALD MONGELA

RC SENYAMULE AMWAPISHA DC MPYA- CHEMBA MHE. GERALD MONGELA

Na Barnabas Kisengi Dodoma Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule amemuapisha Mkuu wa Wilaya ya chimba Mkoani Dodoma uapisho imefanyika Januari 30.2023 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali ya mkoa na wilaya, viongozi wa vyama vya siasa na viongozi wa dini.

Na Barnabas Kisengi Dodoma

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule amemuapisha Mkuu wa Wilaya ya chimba Mkoani Dodoma uapisho imefanyika Januari 30.2023 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali ya mkoa na wilaya, viongozi wa vyama vya siasa na viongozi wa dini.

Akizungumza baada ya uapisho huo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule amewataka wakuu wote wa wilaya kuzingatia na kuheshimu viapo vyao vya utumishi na uadilifu.

“Nawakaribisha sana Dodoma,nawasisitiza mkaendelee kuzisoma kanuni za viapo vyenu ili kuleta ufanisi wa utekelezaji wa majukumu yenu Kwa Serikali na wananchi”amesema Senyamule

Aidha Mhe Rosemary Senyamule amesisitiza swala la utawala Bora,kushughulikia kero za wananchi, ukusanyaji wa mapato, Ustawishaji wa Mazingira, Kushughulikia swala la Elimu bora hususani swala la ufaulu na uandikishaji na upelekwaji wa wanafunzi wa darasa la awali,darasa la kwanza na kidato Cha kwanza.

Hafla hiyo pia imehudhuriwa na Wakuu wa wilaya wote wa wilaya zingine za mkoa wa Dodoma ambao wameendelea kubaki katika vituo vyao vya kazi vya awali Kutoka wilaya za Dodoma Mjini, Kongwa, Chamwino, pamoja na Wakuu wa wilaya waliohamishiwa wilaya za Bahi na Mpwapwa.

Akitoa neno la shukrani mara baada ya kula Kiapo hicho Mkuu Mpya wa wilaya ya Chemba Mhe Gerald Mongela amemshukuru Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan Kumteua kuwatumikia wananchi na serikali wilayani Chemba.

Aidha Mhe Mongela amemwahindi mkuu wa mkoa kuyafanyia kazi maelekezo yake yote na kwamba atafanya kazi Kwa kutumia karma, maarifa,ubunifu na Kwa kuzingatia kiapo chake.

Akizungumza Kwa niaba ya wakuu wa wilaya wote ,Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa aliyehamia Sophia Mfaume Kizigo amemwahidi mkuu wa mkoa utumishi unaozingatia maadili na kwamba Mkoa wa Dodoma ni tunu na fahari ya Watanzania na wao wako tayari Kuwa sehemu ya wanaoienzi na kuistawisha tunu hiyo.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »