Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini asisitiza Ujenzi wa Jengo la Wizara hiyo Uende kwa Kasi

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini asisitiza Ujenzi wa Jengo la Wizara hiyo  Uende kwa Kasi

Na Mwandishi Wetu Dodoma Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo amemtaka Mkandarasi Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuongeza kasi ya ujenzi wa jengo jipya la wizara ili mradi huo ukamilike katika muda uliopangwa  wa kipindi cha miezi 18. Mbibo amesema hayo alipotembelea na kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa ofisi mpya

Na Mwandishi Wetu Dodoma


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo amemtaka Mkandarasi Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuongeza kasi ya ujenzi wa jengo jipya la wizara ili mradi huo ukamilike katika muda uliopangwa  wa kipindi cha miezi 18.


Mbibo amesema hayo alipotembelea na kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa ofisi mpya za Wizara katika mji wa Serikali – Mtumba  Februari 1, 2023 Jijini Dodoma.


Amesema, wizara imetoa msukumo kwa mkandarasi huyo wa mradi na mshauri ili iweze kufanya kazi kwa kasi zaidi na mradi ukamilike kwa wakati katika muda uliopangwa.
Akizungumzia kuchelewa kwa mradi  huo kwa siku 28 amemsisitiza mkandarasi na mshauri kufidia muda uliochelewa wa ujenzi ili kufikia tarehe 14 Aprili 2023 mradi ukamilishwe.
“Tumekuja kuangalia uhalisia wa hatua za ujenzi ambazo zimefikiwa ili kuweza kulinganisha na taarifa ambazo wizara inapokea wizarani na kuijadili na kuangalia namna ya kutoa maamuzi sehemu zilizokwama,” amesema Mbibo.


 Kwa upande wake, Mwakilishi wa Meneja wa Mradi kutoka NHC Nelson Novath amesema, mradi umetoa ajira 162 hadi sasa na wanatarajia kutoa ajira 60 ili kuongeza ufanisi na kufidia muda waliochelewa ili jengo hilo likamilike kwa wakati.


Ziara hiyo imehudhuriwa na Wajumbe wa menejimenti, baadhi ya watumishi wa wizara, na uongozi wa NHC ili kujionea maendeleo ya mradi huo. Mradi huo unatarajiwa kukamilika mwezi Aprili mwaka huu.
 

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »