”Watendaji Wizara ya Maji fanyeni kazi kwa kasi na kwa uadilifu”,Waziri Aweso.

”Watendaji Wizara ya Maji fanyeni kazi kwa kasi na kwa uadilifu”,Waziri Aweso.

Waziri wa Maji Jumaa Aweso  amefungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Sekta ya Maji na amewataka Watendaji Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maji kufanya kazi kwa kasi, uadilifu na uwajibikaji ili lengo la serikali la kutoa huduma bora ya majisafi lifanikiwe hasa akisisitiza kufanyiwa kazi eneo la Takwimu. Waziri Aweso ameainisha kuwa 

Waziri wa Maji Jumaa Aweso  amefungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Sekta ya Maji na amewataka Watendaji Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maji kufanya kazi kwa kasi, uadilifu na uwajibikaji ili lengo la serikali la kutoa huduma bora ya majisafi lifanikiwe hasa akisisitiza kufanyiwa kazi eneo la Takwimu.


Waziri Aweso ameainisha kuwa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt SAMIA SULUH HASSAN  ameonesha nia ya dhati ya kusaidia juhudi za Wizara ya Maji kufikisha huduma ya maji kwa Watanzania,hivyo watendaji wa Wizara wanajukumu la kuhakikisha wanaungana naye kwa kuhakikisha wanakuwa waadilifu na kuratibu matumizi yaliyokusudiwa  ya fedha katika miradi yote ya Maji inayotekelezwa hapa nchini
.

Aidha Waziri wa Maji Jumaa Aweso ametoa tathmini ya wapi sekta ya Maji imetoka, wapi ilipo sasa na mipango ya wapi inaelekea akiyachambua maeneo yalio vizuri na maeneo yenye changamoto na yanayotakiwa kufanyiwa kazi pia akiwapongeza watendaji wa sekta ya Maji kwa kuwa mstari wa mbele kusimamia mageuzi ambayo yamewezesha utekelezaji wa miradi ya maji.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »