Makatibu Tawala fanyeni msawazo wa walimu shule zenye ziada na kuwapeleka shule zenye upungufu zaidi.

Makatibu Tawala fanyeni msawazo wa walimu shule zenye ziada na kuwapeleka shule zenye upungufu zaidi.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais -TAMISEMI, Mhe. David Silinde (Mb) amesema Ofisi ya Rais – TAMISEMI imetoa maelekezo kwa Makatibu Tawala wa Mikoa yote Tanzania Bara kufanya msawazo wa walimu kutoka shule zenye ziada na kuwapeleka katika shule zenye upungufu zaidi. Amesema hayo leo tarehe 08 Februali 2023 Bugeni Dodoma wakati akijibu Swali la Mbunge

May be an image of 4 people, people sitting and indoor

Naibu Waziri Ofisi ya Rais -TAMISEMI, Mhe. David Silinde (Mb) amesema Ofisi ya Rais – TAMISEMI imetoa maelekezo kwa Makatibu Tawala wa Mikoa yote Tanzania Bara kufanya msawazo wa walimu kutoka shule zenye ziada na kuwapeleka katika shule zenye upungufu zaidi.

Amesema hayo leo tarehe 08 Februali 2023 Bugeni Dodoma wakati akijibu Swali la Mbunge viti Maalum, Mhe. Martha Mariki aliyetaka kujua Je, kuna mpango gani wa kutatua changamoto ya uhaba wa Walimu katika shule za pembezoni ?

Mhe. Silinde amesema Serikali imekuwa ikitoa ajira ili kukabiliana na upungufu wa walimu shuleni, unaotokana na walimu kustaafu, kuacha kazi, kufukuzwa, kufariki na ongezeko la idadi ya wanafunzi wanaoandikishwa.

Amesema tangu mwaka 2018/19 hadi mwaka 2021/22, Serikali imeajiri jumla ya walimu 26,598 wakiwemo 16,640 wa Shule za Msingi na 9,958 wa Shule za Sekondari.

Aidha, Mhe. Silinde amesema Serikali ina hakikisha walimu wanaajiriwa na kupangwa katika shule zenye uhitaji zaidi, hususan zilizoko maeneo ya vijijini.

Amesema Ofisi ya Rais – TAMISEMI iliboresha mfumo maalum wa maombi ya ajira na upangaji wa walimu ujulikanao kama Teachers Allocation Protocol (TAP), Kupitia mfumo huo shule zenye upungufu mkubwa wa walimu hususan zilizoko vijijini hubainishwa.

Mhe. Silinde amesema Serikali itaendelea kuajiri walimu kulingana na mahitaji na upatikanaji wa fedha ili kukabiliana na uhaba wa walimu hususani katika maeneo ya pembezoni.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »