TANZIA – Mwili wa aliyekuwa Afisa Habari wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Bathromea Chilwa Chiwiko kuagwa Machi 06 2023 Nyumbani kwake Michese Jijini Dodoma

TANZIA – Mwili wa aliyekuwa Afisa Habari wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Bathromea Chilwa Chiwiko  kuagwa Machi 06 2023 Nyumbani kwake Michese Jijini Dodoma

Na Barnabas Kisengi Dodoma. Chama Cha Waandishi wa Habari mkoa wa Dodoma Center Prees Clabu (CPC) kimepokea kwa masikito makubwa kufuatia kifo cha aliyekuwa  Mwandishi wa Habari na Afisa Habari wa Chama Cha walimu Tanzania CWT Bathromea Chilwa Chiwiko  kilichotokea Jumamosi March 04 2023 katika hospital ya Rufaa ya Benjamini Mkapa Jijini Dodoma. Akizungumza na J

Na Barnabas Kisengi Dodoma.


Chama Cha Waandishi wa Habari mkoa wa Dodoma Center Prees Clabu (CPC) kimepokea kwa masikito makubwa kufuatia kifo cha aliyekuwa  Mwandishi wa Habari na Afisa Habari wa Chama Cha walimu Tanzania CWT Bathromea Chilwa Chiwiko  kilichotokea Jumamosi March 04 2023 katika hospital ya Rufaa ya Benjamini Mkapa Jijini Dodoma.


Akizungumza na J five blog Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari mkoa wa Dodoma CPC Mussa Yusuf amesema wamepokea kwa masikitiko makubwa sana kufuatia taarifa za kifo cha aliyekuwa Mwandishi wa Habari na Afisa Habari wa Chama Cha Walimu Tanzania CWT Bathromea Chilwa Chiwiko aliyefariki Dunia baada ya kupata ajali ya gari Siku ya jumanne katika maeneo ya kivuko cha reli kilichopo kata ya kizota Jijini Dodoma.


Mwenyekiti huyo amesema baada ya kupata taarifa ya kutokea kwa ajali hiyo siku jumanne usiku Bathrome Chilwa Chiwiko alikimbizwa Katika hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na baadaye kuhamishiwa katika hospital ya Rufaa ya Benjamini Mkapa Jijini Dodoma ambako aliendelea kupatiwa matibabu hadi umauti ulipokuta Siku ya Jumamosi March 05 2023 majira ya jioni hospital hapo.
“Marehemu Bathromea Chilwa Chiwiko alikuwa mwenzetu Katika tasnia ya Habari na alikuwa na mchango mkubwa sana kwa Waandishi wa Habari wa mkoa wa dodoma na wanachama wa central prees clabu CPC kwa kutupa ushirikiano mkubwa sana hadi Sasa Bado siamini kama Chilwa ametutoka hapa Duniani” Amesema Mussa Yusuf.


Marehemu Bathromea Chilwa Chiwiko anatarajiwa kuagwa kwa Misa takatifu inayotarajiwa kufanyika Siku ya Jumatatu March 06. 2023 nyumbani kwake michese Jijini Dodoma na kufuatiwa na safari ya kuelekea mpanda Mkoani Rukwa ambako anakwenda kupumzishwa katika nyumba yake ya milele ambapo ibada ya mazishi ya Bathromea Chilwa Chiwiko yatafanyika Siku ya jumanne March 07  2023 Mpanda Mkoani Rukwa.


Marehemu Bathromea Chilwa Chiwiko ameacha mjane moja na watoto wawili  raha ya milele umpe ebwana na mwanga wa milele umwangazie Bathromea Chilwa Chiwiko apumzike kwa Amani.
              “2. Timotheo 4:7”
 Umevipiga vita vilivyo vizuri,mwendo umeumaliza, Imani umeilinda RIP Bathromea Chilwa Chiwiko pumzika kwa Amani Mwamba.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »