Na Mwandishi Wetu Bahi Dodoma Wanawake wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, wamesheherekea siku ya wanawake duniani kwa kukata keki,kupanda miti na kuwapatia mahitaji muhimu wanafunzi wa shule ya msingi Kigwe Viziwi wilayani Bahi mkoani Dodoma.Akizungumza kwa niaba ya wanawake hao, katika shule hiyo, Sylvia Lupembe,amesema katika kusheherekea siku ya wanawake Duniani Watumishi Wanawake

Na Mwandishi Wetu Bahi Dodoma
Wanawake wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, wamesheherekea siku ya wanawake duniani kwa kukata keki,kupanda miti na kuwapatia mahitaji muhimu wanafunzi wa shule ya msingi Kigwe Viziwi wilayani Bahi mkoani Dodoma.Akizungumza kwa niaba ya wanawake hao, katika shule hiyo, Sylvia Lupembe,amesema katika kusheherekea siku ya wanawake Duniani Watumishi Wanawake wa Wizara hiyo wameamua kusheherekea na wanafunzi hao kwa kukata keki pamoja nao.
Amesema kuwa pamoja na kukata keki wamekabidhi vifaa mbalimbali katika shule hiyo ambavyo ni Simtank lita 4000, Mashuka, Mipira ,Taulo za kike,Magodoro, Juice, Biscuit ,keki“Tumekuja kama wazazi,walezi na wenzao kwa sababu ni eneo letu la kisera,tumekuja kuwaona na kuwatia moyo kwamba wanaweza na wapo shule wanaweza,”amesema Lupembe.
Amesema Wizara inasaidia kwa kuwekeza kiasi kikubwa kuhakikisha kuna kuwa na miundombinu rafiki ya wao kuweza kupata elimu.“Leo tumekuja na mahitaji ambayo waliyataja wao wenyewe tumewaletea magodoro ambayo yatawafanya walale kwenye mazingira rafiki lakini tumewaletea mashuka na Matanki ya maji pamoja na taulo za kike kwa watoto wa kike,”amesema LupembeAmesema kwa sababu wapo katika msimu wa sherehe wameenda kufurahi pamoja na kula keki na wamepanda miti kwa pamoja na wanafunzi hao.“Mwaka huu wanawake tunasheherekea kwa kudhamini ubunifu teknolojia na sisi tumesikia kutoka kwao kwamba wanahitaji vifaa vya tehama vikiwemo Vishkwambi eneo hili tunaliona ni la kimkakati tunatakiwa kulifanyia kazi,”amesema Lupembe.
Amesema wanafurahi kuona wanafunzi hao wanafundishwa malezi na stadi za maisha ambazo zitakuja kuwasaidia katika maisha yao.“Sisi kama Wanawake tunasema tumetumia nguvu zetu na kidogo tulichokipata kula na kufurahi na watoto wetu,”amesema Lupembe.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule Kigwe Viziwi Thadei Mhwagila amesema wanashukuru watumishi wanwake wa wizara ya Elimu kwa ugeni huo kwani wanafunzi wamefurahi.
Amesema Watumishi Wanawake whao wamewajengea upendo ambao wanahisi walikuwa wanaukosa katika maeneo wanayoishi.“Tunapenda kushukuru kwa hicho wametoa msaada mkubwa kwa sababu watoto hawa wanaishi na Bibi zao mara nyingi wanakosa mahitaji ya msingi,”amesema MhwagilaHata hivyo ametoa ushauri kwa wazazi na walezi kuwaona watoto wote wapo sawa na kuwathamini watoto hao.
“Nitoe shukrani kwa Serikali kwa kuwajali hawa watoto wametuletea fedha kujenga mabweni wataishi katika mazingira mazuri,”amesema MhwagilaNaye,Afisa Elimu,Elimu Maalum,Idara ya Elimu Msingi,Wilaya ya Bahi,Sarah Chizingwa amewashukuru Wanawake wa Wizara ya hiyo kwa kutoa misaada hiyo na kuwaona watoto hao.
“Tunafurahi kwa upendo mliotuonesha sisi kwa kuja kuwaona wototo wetu wenye ulemavu ambao ni viziwi tumepokea zawadi zenu na Mungu awabariki pale mlipuoungukiwa Mungu awaongezee tunawakaribisha wakati mwingine Bahi,”amesema Chizin
Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *