Mkoa wa Tabora umepokea zaidi ya shilingi Billion 21 kwaajili ya kuboresha huduma za afya

Mkoa wa Tabora umepokea zaidi ya shilingi Billion 21 kwaajili ya kuboresha huduma za afya

Na. Catherine Sungura, WAF-Tabora TABORA YAPOKEA ZAIDI YA SHILINGI  BILIONI 21 NDANI YA MIAKA MIWILI YA RAIS SAMIA Awamu ya sita chini ya Uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya kuboresha huduma za afya kwa Mkoa wa Tabora. Hayo yamesemwa leo na Katibu Tawala wa Mkoa

Na. Catherine Sungura, WAF-Tabora


TABORA YAPOKEA ZAIDI YA SHILINGI  BILIONI 21 NDANI YA MIAKA MIWILI YA RAIS SAMIA Awamu ya sita chini ya Uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya kuboresha huduma za afya kwa Mkoa wa Tabora.


Hayo yamesemwa leo na Katibu Tawala wa Mkoa huo Dkt. John Mboya wakati akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora kwenye uzinduzi wa huduma za kibingwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora-Kitete ambapo huduma hizo zitatolewa kwa siku 5 na Madaktari bingwa kutoka hospitali za rufaa za Mikoa ya Amana, Temeke na Tumbi. 
“Napenda kuipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya Uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa maboresho makubwa ambayo yamefanyika katika mkoa wetu wa Tabora na katika hospitali yetu hii ya rufaa ya Mkoa Tabora-Kitete”.
“Kwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora- Kitete,Serikali ilitupatia fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo la wodi ya wazazi, jengo la huduma za uchunguzi (mionzi), jengo la huduma za wagonjwa mahututi (ICU), nyumba ya watumishi pamoja na ukarabati wa jengo kwaajili ya Tiba mtandao”.


Amesema jumla ya fedha kiasi cha shilingi Bilioni 6.6 zimetumika katika ujenzi wa majengo hayo pamoja na vifaa Tiba vipya na vya kisasa vitakavyowekwa, pia mapokezi ya vifaa tiba vya kisasa, ambapo moja kati ya vifaa Tiba hivyo ni CT-SCAN yenye thamani ya shilingi bilion 1.8 kwa ajili ya kuendelea kuboresha huduma kwa wagonjwa.

Kwa ujio wa Madakatari bingwa hao Katibu Tawala huyo amewataka wananchi wa Mkoa wa Tabora kujitokeza kwa wingi  kuweza kupatiwa huduma za matibabu ya kibingwa  bila malipo ili kuweza kuwapunguzia gharama ambazo awali walikuwa wakizitumia kwa kufuata huduma hizo nje ya mkoa  kwenye hospitali ya Taifa na zile za kanda.


Aidha, amesema ujio wa madaktari hao ni njia ya kujengewa uwezo madaktari  ambao ni waajiriwa katika hospitali  ya Kitete katika swala zima la utoaji wa huduma bora kwa wateja wa mkoa huo.
“Hivyo nitoe wito kwa madaktari wetu waliopo katika hospitali hii ya kitete kushiriki kikamilifu katika zoezi la kuwaona wagonjwa kwa kushirikiana na madaktari bingwa hawa ili watakapo ondoka basi ujuzi na taaluma vibaki kwa madaktari wetu” Amesema Dkt. Mboya.
Naye, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Honoratha Rutatinisibwa amewashukuru Madaktari bingwa hao kwa ujio wao ambao utawasaidia wananchi wa Tabora ambao wangepata rufaa ya kwenda Bugando, KCMC, Muhimbili au Benjamin Mkapa.

Dkt. Rutatinisibwa amesema kuwa Mkoa wa Tabora unakabiliwa na uhaba wa madaktari bingwa wa fani mbalimbali ambopo kwa sasa mkoa una madakatari bingwa 7 wakati mahitaji ni madaktari sabini na tano (75) na kuongeza kuwa Mkoa kuna mahitaji makubwa kwa wananchi kupata hduma hizo za Kibingwa.
Awali Mfadhili wa ujio huo wa madaktari bingwa Bw. Jafary Mnete wa kampuni ya Master Card amesema afya ndio mtaji kwa mwanadamu yeyote hivyo kampuni yao imeona umuhimu wa kuwafikishia huduma hizo wananchi wa Tabora ili kuweza kuwaondolea adha ya kufuata huduma za kibingwa nje ya mkoa huo.


Nao wananchi wa Mkoa wa Tabora wameishukuru Wizara ya Afya kupitia Hospitali ya Rufaa ya Tabora-Kitete kwa kuwafikishia huduma za Kibingwa katika mkoa wao na hivyo kuwasaidia kuwapunguzia gharama za matibabu pamoja na rufaa za kuzifuata huduma hizo nje ya mkoa huo.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »