TANZANJA YATOA MISAADA JANGA LA KIMBUNGA FREDDY NCHINI MALAWI

TANZANJA YATOA MISAADA JANGA LA KIMBUNGA FREDDY NCHINI MALAWI

Na Moreen Rojas Dodoma Serikali ya Jamuhuru ya Muungano wa Tanzania Imetoa misaada mbalimbali kwa nchi ya Malawi kufuatia nchi hiyo kukumbwa na janga la dhoruba la kimbunga kijulikanacho kama “Tropiki Freddy”. Mkurugenzi wa habari na uhusiano wa jeshi la ulinzi na uhusiano wa jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Kanali Gaudentius

Na Moreen Rojas Dodoma


Serikali ya Jamuhuru ya Muungano wa Tanzania Imetoa misaada mbalimbali kwa nchi ya Malawi kufuatia nchi hiyo kukumbwa na janga la dhoruba la kimbunga kijulikanacho kama “Tropiki Freddy”.


Mkurugenzi wa habari na uhusiano wa jeshi la ulinzi na uhusiano wa jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Kanali Gaudentius Ilonda amesema hayo wakati akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari Jijini Dodoma Marchi 18 2023.


Luteni Ilonda amesema kufuatia kutokea kwa kimbunga hicho kimesababisha maafa makubwa kiasi cha kutangazwa kuwa janga katika nchi ya Malawi na kusababisha vifo, kuharibu miundombinu mbalimbali, nyumba, mazao na athari nyingine nyingi nchini hapo.
” Kama mtakumbuka vizuri Marchi 13  2023 kulitokea na kimbunga kiitwacho’Tropiki Freddy’ kilichoambatana na mvua kubwa na upepo mkali kiliikumba nchi ya malawi,kiasi cha kutisha cha maji yalitiririka katika vitongoji na kusomba nyumba na kuleta maafa “Amesema Luteni Kanali Ilonda.


Aidha kufuatia janga hilo,serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kutambua ujirani mwema,ushirikiano na udugu wetu na nchi ya malawi hivyo serikali imetoa misaada mbalimbali ya kibinadamu ili kuisaidia nchi hiyo kukabiliana na janga hilo hivyo jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania limepewa dhamana ya jukumu kushiriki bega kwa bega kupeleka misaada mbalimbali kutoka nchini Tanzania.


Luteni kanali Ilonda Amesema kufuatia jukumu hilo Mkuu wa majeshi Jenerali Jacob John Mkunda ametoa maelekezo yanayoratibiwa na mnadhimu mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania JWTZ Luteni Jenerali Salum Haji Othman la kusafirisha misaada hiyo kwa kutoa magari ya JWTZ zaidi ya 37 yataondoka Dodoma muda wowote kuanzia hivi sasa kuelekea nchini Malawi.
“Baadhi ya magari hayo yanayopelekwa malawi ni pamoja na gari la wagonjwa(ambulance),karakana tembezi ya magari (mobile workshop) na malori makubwa yenye uzito wa tani 30 idadi ishirini 20 na malori yenye uzito wa tani zaidi ya kumi na name(18) idadi 10”


Aidha amesema kuwa magari hayo yatasafirisha misaada wa mahema,mablanketi,chakula na mahitaji mengine ya kibidamu yanayotolewa na serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Sambamba na hilo Luteni kanali Ilonda Amesema JWTZ imepeleka helikopta mbili  ikiwa ni sehemu ya msaada unaotolewa na serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania kusaidia janga hilo nchini Malawi na hivi punde helikopta hizo zimeruka kutokea Dar es Salaam kuelekea Malawi tayari kuanza utekelezaji wa majukumu hayo.


Aidha ametoa rai kwa wananchi kuwa watulivu wakati zoezi hilo linaendea wananchi wasiwe na taharuki kwa vile wataona magari mengi yakiingia Malawi wakati zoezi hilo likiwa linaendelea.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »