TRA yawafikisha Mahakamani Wakurugenzi kwa Makosa ya kikodi

TRA yawafikisha Mahakamani Wakurugenzi kwa Makosa ya kikodi

Na Barnabas Kisengi Dodoma Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mkoa wa Dodoma limewafikisha mahakamani   Wakurugenzi Watatu wa Kampuni ya Corsyne Consult Limited kwa makosa matatu ya kikodi ikiwemo kutengeneza risiti bandia za kielektroniki na kuisababishia serikali hasara ya sh.milioni 100.7. Akizungumza na wandishi wa habari  jijini Dodoma Ofisa Sheria wa TRA Mkoa wa Dodoma, Erasto

Na Barnabas Kisengi Dodoma


Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mkoa wa Dodoma limewafikisha mahakamani   Wakurugenzi Watatu wa Kampuni ya Corsyne Consult Limited kwa makosa matatu ya kikodi ikiwemo kutengeneza risiti bandia za kielektroniki na kuisababishia serikali hasara ya sh.milioni 100.7.

Akizungumza na wandishi wa habari  jijini Dodoma Ofisa Sheria wa TRA Mkoa wa Dodoma, Erasto Mtondokoso amesema washtakiwa  hao walitenda makosa kati ya Julai hadi Disemba mwaka jana 2022 na kufanikiwa kutengeneza risiti bandia  22 za vifaa vya ujenzi.

Mtondokoso ameyataja Makosa mengine ni pamoja na ulipaji wa kodi na matumizi yasiyo halali ya Mashine za kutolea risiti za kielektroniki.
“Kwa leo tumefanikiwa kumsomea shtaka mshtakiwa wa kwanza ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo na Mkazi wa Mwanza Biswalo Peter Biswalo (38) ambaye hajakiri kutenda kosa hilo,”amesema.

Amewataja washtakiwa wengine kuwa ni Denisi Kisoka (38) na Ezekieli mayunga ambao wote ni wakazi wa Mkoa wa Mwanza.

Kwa upande wake Meneja wa Idara ya Upelelezi wa Kodi Kanda ya Kati Nicholous Njovu amesema watuhumiwa hao wamekuwa wakitengeneza risiti bandia ili kukwepa kulipa kodi.


Pamoja na mambo mengine amewataka wafanyabiashara wanaohujumu serikali kwa kutoa risiti bandia kuwa TRA wako macho na imeimarisha mifumo yake kuhakikisha inawanasa watuhumiwa wote wanaokwepesha mapato ya serikali
“Natoa rai kwa wote waliokuwa na mpango wa kutengeneza risiti bandia waache mara moja, na wananchi wanatakiwa kudai risiti za kielekroniki  pindi wanapofanya manunuzi,”alieleza.


Licha ya hayo  Njovu amewataka wananchi kuhakiki risiti wanazopewa kama ni halisi au bandia kwa kutumia simu zao za mkononi ama kufika katika ofisi za TRA kuuliza.
Kwa mujibu wa Wakili Tondokoso amebainisha kuwa washtakiwa wengine watasomewa mashtaka Aprili 6 2023 mwaka huu.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »