TULINDE MAADILI YA VIZAZI VYA SASA NA VIJAVYO-RAIS DK.MWINYI.

TULINDE MAADILI YA VIZAZI VYA SASA NA VIJAVYO-RAIS DK.MWINYI.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Dunia kwa sasa inakabiliwa na changamoto za harakati kuhusu kupenyeza uharibifu wa maadili hivyo kupitia utaratibu wa mashindano ya kuhifadhi Qur’aan ni jitihada za kuimarisha maadili mema kwa kuwalea vijana kiroho na kitabia. Ameyasema hayo leo tarehe 16 Aprili 2023 katika

Inaweza kuwa picha ya Watu 4 na jukwaa
Inaweza kuwa picha ya Watu 4 na jukwaa
Inaweza kuwa picha ya Watu 5 na jukwaa
Inaweza kuwa picha ya mtu mmoja au zaidi
Inaweza kuwa picha ya Watu 6 na jukwaa
Inaweza kuwa picha ya Watu 3 na jukwaa

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Dunia kwa sasa inakabiliwa na changamoto za harakati kuhusu kupenyeza uharibifu wa maadili hivyo kupitia utaratibu wa mashindano ya kuhifadhi Qur’aan ni jitihada za kuimarisha maadili mema kwa kuwalea vijana kiroho na kitabia.

Ameyasema hayo leo tarehe 16 Aprili 2023 katika fainali za Tuzo za Kimataifa za Qur’aan zilizoandaliwa na Jumuiya ya kuhifadhi Quran Tanzania ukumbi wa diamond Jubilee , Dar es Salaam .

Aidha Rais Dk.Mwinyi amewahimiza Vijana waumini wa dini ya Kiislamu kuisoma Quran na kushikamana kupitia mafunzo yake kwa kuleta tija kwa jamii na kuendelea kuyalinda maadili mema Kizazi cha sasa na kijacho.

Mashindano hayo ya Tuzo za kimataifa za Quran Mwaka 2023 yametimiza miaka 31 tangu kuanzishwa kwake yameshirikisha nchi zaidi ya kumi na tisa kutoka mabara tofauti na washiriki maalumu wa Adhana kutoka nchi tatu.

Pia amemkabidhi zawadi kwa mshindi wa Kwanza Galal Saaed kutoka Yemen dola za Kimarekani elfu tano. Mshindi wa pili Abubaker Sharif kutoka Sweden dola za Kimarekani elfu nne. Mshindi wa tatu Abdul Biro kutoka Tanzania dola za Kimarekani elfu tatu.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »