SERIKALI ITABORESHA UPATIKANAJI WA DAWA,VIFAA TIBA,VITENDANISHI NA MIFUMO YA HUDUMA ZA AFYA.

SERIKALI ITABORESHA UPATIKANAJI WA DAWA,VIFAA TIBA,VITENDANISHI NA MIFUMO YA HUDUMA ZA AFYA.

Serikali imesema itaendelea kuweka mifumo itakayowezesha uagizaji wa vitendanishi, vifaa tiba na dawa kwa Halmashauri zote ili kuboresha huduma za afya ya msingi nchini. Akijibu hoja za Waheshimiwa Wabunge tarehe 18 Aprili, 2023 Bungeni Jijini Dodoma Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mheshimiwa Angellah Kairuki amesema Serikali itaendelea kufanya vikao na Wizara ya Afya

Serikali imesema itaendelea kuweka mifumo itakayowezesha uagizaji wa vitendanishi, vifaa tiba na dawa kwa Halmashauri zote ili kuboresha huduma za afya ya msingi nchini.

Akijibu hoja za Waheshimiwa Wabunge tarehe 18 Aprili, 2023 Bungeni Jijini Dodoma Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mheshimiwa Angellah Kairuki amesema Serikali itaendelea kufanya vikao na Wizara ya Afya ili kujadiliana namna ya kuwasilisha vitendanishi, vifaa, vifaa tiba na dawa pamoja na kuweka mifumo itakayowezesha uagizaji wa vitendanishi, vifaa tiba na dawa kwa ajili ya Halmashauri zote nchini.

Kuhusu mafunzo ya Watendaji wa Kata na Vijiji, Waziri Kairuki amesema Ofisi ya Rais – TAMISEMI inaratibu mafunzo ya awali na mafunzo ya utumishi wa Umma, usalama na huduma kwa jamii kwa Maafisa hao katika Chuo cha Utumishi wa Umma ili kuongeza uwajibikaji wa watumishi ambapo kwa mwaka 2022/23 Watendaji wa Kata 1,936 watapatiwa mafunzo kwa awamu.

Kuhusu uhaba wa madawati kwenye shule za Msingi na Sekondari, Waziri Kairuki amesema utengenezaji wa madawati umekuwa ukitekelezwa sambamba ujenzi wa vyumba vya madarasa kupitia vyanzo mbalimbali vya mapato kama vile Serikali Kuu, wadau pamoja na miradi mbalimbali ya maendeleo na mwaka 2021/22 jumla ya madawati 794,000 yametengenezwa katika shule za Sekondari kupitia fedha za UVIKO-19, Tozo za miamala ya Simu, EP4R na SEQUIP.

Serikali imeendelea kuhamasisha Wadau wa Elimu kote nchini kuendelea kuchangia katika ujenzi wa miundombinu ya elimu ikiwemo utengenezaji wa madawati ili kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »