Sekta ya utalii itakuwa sekta mama ya uchumi wa Zanzibar.

Sekta ya utalii itakuwa sekta mama ya uchumi wa Zanzibar.

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema ina azma ya kuendeleza nakufikia hatua kubwa zaidi kuifanya sekta ya utalii kuendelea kuwa sektamama ya uchumi wa Zanzibar kwa miaka mitatu ijayo.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyiameyasema hayo kwenye mkutano na wahariri na waandishi wa habari kutokavyombo mbalimbali vya habari, Ikulu,

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema ina azma ya kuendeleza na
kufikia hatua kubwa zaidi kuifanya sekta ya utalii kuendelea kuwa sekta
mama ya uchumi wa Zanzibar kwa miaka mitatu ijayo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi
ameyasema hayo kwenye mkutano na wahariri na waandishi wa habari kutoka
vyombo mbalimbali vya habari, Ikulu, Zanzibar ikiwa ni kawaida yake ya
kuzungumza nao kila mwisho wa mwezi.
Dk. Mwinyi alisema sekta ya Utalii Zanzibar, inachangia asilimia 30 pekee ya pato
la uchumi wa Zanzibar, ikilinganishwa na sekta nyengine za Maendeleo, kupitia
utalii wa Fukwe, Bahari na Mji mkongwe, umeongeza watalii wengi kiasi ya
wawekezaji kuendelea kujenga hoteli nyingi kubwa pamoja na nyumba za wageni
za kisasa.
Aidha, Rais Dk. Mwinyi aliendelea kusisitiza umuhimu wa Zanzibar kuwa na utalii
wa kumbi za mikutano na kueleza kuwa ni chachu ya kukuza uchumi wa nchi na
kuongeza haraka fursa za biashara kwa Serikali, taasisi binasi na wananchi wa
kawaida, akitolea mfano wa mkutano mkubwa wa Chama cha Menejimenti ya
Makatibu Mahsusi (TAPSEA) na Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na
Nyaraka (TRAMPA) uliofanyika Mei 27 mwaka huu maeneo ya Fumba, Zanzibar.
Rais Dk. Mwinyi alisema, kupitia mkutano huo, Wananchi kutoka maeneo
mbalimbali ya bara na visiwani kutoka sekta za umma walikusanyika pamoja
kujadili masuala yao, hali iliyotoa fursa nyingi za uchumi na biashara zikiwemo,
nyumba za wageni kupokea wageni wengi, vyombo vya usafiri wakiwemo
bodaboda, taxi, na aina nyengine za usafiri, hoteli, wafanyabiashara wa vyakula,
matunda na wenyeji wa eneo lililowakutanisha washiriki wa mkutano huo kwa
namna moja ama nyengine walinufaika na fursa hizo.
“Ndio maana naendelea kuwasisitiza wananchi wa Kilimani kuangalia kwa upana
wa faida za utalii wa mikutano na fursa zake ili wachangamkie fursa hizo zenye
nia ya kuleta mabadiliko makubwa ya uchumi na maendeleo” aliweka misisitizo
Dk. Mwinyi.
Alisema, ikitoka sekta ya mafuta na gesi kuibuka na kukua ghafla itachukua nafasi
ya sekta ya utalii, kwani duniani kote mafuta na gesi ndio seka kiongozi ya
uchumi.
Akitoa ufafanuzi kuhusu ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa hesabu za Serikali,
aliyodaiwa kuiopokea kwa siri na kutoitangaza kwa umma, Rais Dk. Mwinyi
aliwatoa hofu wananchi na kueleza kwa mujibu wa sheria lazima ripoti iwasilishwe
mapema Baraza ya Wawakilishi na bahati baraza lililkua limeanza hivyo, kulikuwa
na haja ya kuwasilishwa mapema barazani na baadae taratibu nyengine za
kuitangaza zitafuata wiki ijayo.
“Wakati ripoti ya CAG inakuja kwangu, kuna utaratibu wa kisheria kwamba Baraza
la Wawakilishi likinza ndani ya wiki moja, siku saba, lazima ripoti ya CAG iwe
imeshapelekwa na kwa ratiba na safari tulizokuwa nazo tukasema wacha

tuipokee, tumkabidhi Waziri husika aiwasilishe Barazani ndani ya kipindi hicho
tusije tukavunja utaratibu wa kisheria” Alifafanua Dk. Mwinyi.
Alieleza ni kweli Baraza limeanza, ripoti ilipelekwa na tayari imepangiwa siku ya
kusomwa hadharani.
Akitolea ufafanuzi wa baadhi ya maswali aliyoulizwa kwenye mkutano huo kuhusu
ripoti ya CAG, yaliyowahusu baadhi ya wasaidizi wake wakimwemo mawaziri na
watendaji wengine wa Serikali endapo ripoti hiyo itawakuta na ubadhirifu ndani ya
Serikali anayoiongoza, Rais DK. Mwinyi alieleza, kuna njia tatu za kuwachukulia
kwanza ni hatua za kuitawala, ambapo Serikali ikimgundua muhusika amehusika
na uzembe fulani, kutoka kwenye ripoti ya CAG atatolewa Serikalini.
Lakini pia Rais Dk. Mwinyi alieleza njia nyengine ya jinai ambapo Serikali haihusiki
sana, ikitokea mmoja wa wasaidizi wake amekamatwa na ubadhirifu basi moja
kwa moja atapelekwa mahakamani nakueleza kwamba wapo baadhi yao wana
kesi mahakamani kutokana na kukutwa na ubadhirifu kwenye ripoti ya CAG kwa
nyakati zilizopita.
Kuhusu changamoto za ubovu na uchakavu wa barabara nyingi za mjini na vijini,
Dk. Mwinyi alieleza Serikali imezamiria kuzifanyia matengenezo makubwa
barabara zote kwa kujibu wa viwango vya maeneo.
Alisema barabara za Mjini zitatofautiana na za mashamba kwa viwango na uimara
licha ya zote kutarajiwa kuwa kwenye uimara wa hali ya juu lakini zitatofautiana
kwa mujibu wa matumizi ya bara bara hizo pamoja na madaraja na barabara za
juu.
Nakueeleza kwamba barabara inayoelekea bandari jumuishi ya Mangapwani
itakua yakiwango cha hali ya juu zaidi kwa mujibu wa matumizi yake ya shughuli
za bandari.
Akizungumzia Ujenzi wa bandari Jumuishi ya Mangapwani, Rais Dk. Mwinyi
alieleza lengo la bandari hiyo ni kuhudumia kanda nzima ya Afika Mashariki sio
Zanzibar pekee.
Alieleza awali utaratibu wake ulianza mazungumzo na watu wa Oman, kisha
Serikali ilizungumza na watu kutoka Abu Dhabi, alieleza majadiliano hayo
yanafanywa baina ya timu ya serikali yenye nia ya kupata mkataba utakaokuwa na
maslahi ya nchi na bandari itakayojengwa kwa mujibu wa matakwa ya Serikali
ambayo lazima yazingatie sehemu za makontena, mafuta, nafaka, mafuta na gesi
eneo huru (Free zone na masuala ya kilojistiki)
Aidha, alieleza Serikali inatarajia kuyapandisha hadhi, maeneo ya Mangapwani na
Bumbwini kuwa miji mikubwa ya bandari.
Hata hivyo, Rais Dk. Mwinyi pia alitoa ufafanuzi kufuatia safari yake ya kikazi mjini
Doha, Qatar aliyoifanya hivi karibuni na kuwaelezea waandishi wa habari kwenye
mkutano huo alivyopata fursa kueleza maeneo mbalimbali ya biashara na
uwekezaji yanayopatikana Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

IDARA YA MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »