Mke wa Rais, Mariam Mwinyi amesema michezo inajenga Afya.

Mke wa Rais, Mariam Mwinyi amesema michezo inajenga Afya.

Mke wa Rais wa Zanzibar mama Mariam Mwinyi amesema michezo ina nafasi kubwa  katika kujenga mwili na kulinda afya dhidi ya  maradhi mbali mbali. Akizungumza katika Bonanza  liloandaliwa na umoja wa wanawake wilaya ya Amani Mama Mariam amesema ikiwa wananchi watajenga  utamaduni kushiriki michezo na kufanya mazoezi kutasaidia kujikinga magonjwa mbali mbali . Amesema kumekuwa

Mke wa Rais wa Zanzibar mama Mariam Mwinyi amesema michezo ina nafasi kubwa  katika kujenga mwili na kulinda afya dhidi ya  maradhi mbali mbali.

Akizungumza katika Bonanza  liloandaliwa na umoja wa wanawake wilaya ya Amani Mama Mariam amesema ikiwa wananchi watajenga  utamaduni kushiriki michezo na kufanya mazoezi kutasaidia kujikinga magonjwa mbali mbali .

Amesema kumekuwa na maradhi mengi yanayoleta athari kwa wananchi wengi  ikiwemo shindikizo la damu ambayo kwa kiasi kikubwa huchangiwa na kutofanya mazoezi mara kwa mara.

Katika hatua nyengine Mama Mariam Mwinyi amewapongeza umoja wa wanawake wilaya ya Amani kwa kuongeza idadi ya wanachama wapya 200 ambao watakwenda kukitumikia chama katika harakati za kukiletea maendeleo.

Naibu katibu mkuu jumuiya ya kina mama Tunu Juma Kondo, amesema jumuiya imeridhishwa na kasi ya maendeleo yanayofanywa na Raisi wa Zanzibar katika kuimarisha miundombinu ya afya maji na elimu .

Mwenyekiti  umoja wa wanawake wilaya ya Amani Fransisca Camil , amesema jumuiya hiyo itaendelea  kutekeleza majukumu yake kwa kuengeza idadi ya wanachama wapya.

Bonanza lilo liloandaliwa na umoja wa wanawake wa wilaya ya Amani limejumuisha michezo mbali mbali ikiwemo mchezo wa nage, mashindano ya kula maandazi, kufukuza kuku ,kuvuta kamba na mchezo wa mpira wa miguu kwa wanawake ambapo timu ya new generation imebuka na ushindi wa mabao 2 kwa 0 dhidi ya grean queen, bonanza ambalo limefanyika katika viwanja vya Sebleni kwa Wazee.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »