CCM imedhamiria kuwawezesha watendaji wake kiuchumi.

CCM imedhamiria kuwawezesha watendaji wake kiuchumi.

CHAMA Cha Mapinduzi, CCM kimesema kimedhamiria kuwawezeshawatendaji wake kiuchumi ikiwemo kuwalipa posho la kila mwezi mabalozi wangazi zote za ChamaMakamu Mwenyekiti wa Chama hicho,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. HusseinAli Mwinyi ameyasema hayo Ukumbi wa  Umoja ni nguvu, Wilaya ya Mkoanikatika ziara yake ya Chama kisiwani Pemba.Dk. Mwinyi alisema, Chama

CHAMA Cha Mapinduzi, CCM kimesema kimedhamiria kuwawezesha
watendaji wake kiuchumi ikiwemo kuwalipa posho la kila mwezi mabalozi wa
ngazi zote za Chama
Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein
Ali Mwinyi ameyasema hayo Ukumbi wa  Umoja ni nguvu, Wilaya ya Mkoani
katika ziara yake ya Chama kisiwani Pemba.
Dk. Mwinyi alisema, Chama pia kimekusudia kuimarisha Miundombinu ya
ofisi zake zote ikiwemo vitendea kazi, huduma za stationari, vyombo vya usarifi
kwaajili ya kazi za chama.
Makamu Mwenyekiti Dk. Mwinyi alimuagiza Naibu Katibu Mkuu CCM
Zanzibar, Muhamed Said Dimwa, kuanza kutoa vitambulisho vya mabalozi
kwaajili ya kulipiwa posho la kujikimu la kila mwezi.
Aidha, alieleza kadi kuweka utaratibu mzuri wa kuwatambua wanachama wake
kielekroniki.
Pia, aliahidi kusimamia vyema rasilimali za Chama ili zitumike, katika
kukiimarisha.
Pamoja nakuahidi kujenga kumbi kubwa za kisasa za mikutano kwa Unguja na
Pemba zenye uwezo wa kubeba mikutano mikuu ya Chama kitaifa.
Kuhusu utekelezaji Ilani ya uchaguzi ya CCM, 2020- 2025, Dk. Mwinyi,
alieleza  ndani ya kipindi cha miaka miwili na nusu tayari miradi mingi ya
maendeleo imekamilika na kuongeza juhudi  zaidi kwenye kuimarisha
miundombinu ikiwemo barabara, ujenzi wa uwanja wa ndege wa kisasa wa
Pemba utakaojumuisha barabara ya kilomita 2.5 pamoja na jengo jipya la abiria
ili kukifungua kisiwa kwa uwekezaji, utalii na kutoa ajira mpya kwa wananchi
wa Pemba.
Aliongeza ujenzi wa bandari za Mkoani na Wete katika kuifungua Pemba
kiuchumi  kwa meli za mizigo za kimataifa kuingia moja kwa moja ili
kupunguza gharama za bidhaa nchini, hata hivyo, alieleza tayari upembuzi
yakinifu umefanyika.

Alieleza, hatua hiyo itawavutia wawekezaji kujenga viwanda na kuzalisha
bidhaa zao nchini kwani Pemba ina maeneo huru ya uwekezaji.
Dk. Mwinyi amewatoa hofu wananchi wa Pemba kwa kuwaondolea shida ya
upatikanaji wa maji Safi na kueleza tayari imejenga matangi ya maji pamoja na
kusambaza maomba nchi nzima, mijini na vijijini.
Akizungumzia sekta ya Elimu Rais Dk. Mwinyi alieleza Serikali imejenga skuli
za kisasa za ghorofa za msingi na sekondari, aidha, aliahidi kujenga madarasa
2000 Kila mwaka.
Sambamba na kujenga vituo vipya vya Afya na kuimarisha Miundombinu ya
kisasa kwa hospital zote wilaya ikiwemo maabara za kisasa, huduma za vipimo 
pamoja na ujenzi wa hospitali ya rufaa na kuiboresha hospitali kuu ya Abdalla
Mzee.
Dk. Mwinyi pia alimuagiza Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar, kuwapa elimu
viongozi wapya wa chama pamoja na  kutayarisha mpango maalumu
kuwajuulisha viongozi kujua majukumu yao, aidha, aliwaagiza kufanya vikao
vya kikatiba ili kushughulikia mapema changamoto za wananchi.
Naye, Naibu Katibu Mkuu CCM, Zanzibar, Mohammed Said Dimwa
aliwaagiza makatibu wake wa chama, viongozi wakuu wa majimbo, Wabunge
na Wawakilishi ili kutatua haja za wananchi.
Akitoa salamu za Mkoa wa Kusini Pemba, Mkuu wa Mkoa huo, Zahor Matar
alieleza kipindi cha miaka miliwi ya uongozi wa Dk. Mwinyi ametekeza
maendeleo kwa asilimia 85 kwa sekta zote za maendeleo ikiwemo Afya, maji,
Elimu, miundombinu, ustawi wa jamii, Uchumi wa buluu na michezo kwa
kijengwa viwanja vya michezo kwa Wilaya zote za Pemba.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »