RAIS MWINYI AMEIPONGEZA TAASISI YA BENJAMIN MKAPA KWA UWEKEZAJI.

RAIS MWINYI AMEIPONGEZA TAASISI YA BENJAMIN MKAPA KWA UWEKEZAJI.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amewapongeza wajumbe wa Bodi na Menejimenti ya Taasisi ya Benjamin William Mkapa (BMF) na kampuni tanzu Imara Horizon kwa fikra sahihi za uwekezaji wa jengo la Benjamin William Mkapa Health Plaza .Rais Dk. Mwinyi ambaye pia ni Msarifu wa Taasisi hiyo amesema kwa

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amewapongeza wajumbe wa Bodi na Menejimenti ya Taasisi ya Benjamin William Mkapa (BMF) na kampuni tanzu Imara Horizon kwa fikra sahihi za uwekezaji wa jengo la Benjamin William Mkapa Health Plaza .
Rais Dk. Mwinyi ambaye pia ni Msarifu wa Taasisi hiyo amesema kwa hatua ya uwekezaji wa jengo hilo ambalo litakuwa linatoa huduma za afya na ofisi kwa mashirika ya afya ni kielelezo kimojawapo cha mafanikio na kutimiza maono ya kumuenzi Hayati Benjamin William Mkapa.
Ameyasema hayo leo katika hafla fupi ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la Benjamin William Mkapa Health Plaza lililopo Kawe Jijini, Dar es Salaam. 
Aidha, Rais Dk.Mwinyi amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zinaendeleza jitihada za kuongeza uwekezaji katika sekta ya Afya hususan katika ujenzi wa miundombinu, ununuzi wa vifaa tiba na upatikanaji wa watumishi wa sekta ya Afya.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Godwin Mollel akimwakilisha Waziri wa Afya Ummy Ali Mwalimu katika Hafla hio,amesema tuna kazi kubwa ya kutengeneza kizazi kijacho kazi ambayo pia itafanywa ndani ya Jengo hilo litakapokamilika ili kupata wataalamu kwa kupitia Bongo zetu.
Nae Dk.Ellen Mkondya-Senkoro ambae ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa (BMF)akaelezea mafanikio yaliyopatikana chini ya Taasisi ya Mkapa Tangu Rais Dk.Mwinyi alivyochaguliwa kuiongoza akiwa Msarifu ndani ya taasisi hio.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »