LAKE AGRO WAFADHILI UPASUAJI WA NGIRI MAJI (MABUSHA) RUFIJI

LAKE AGRO WAFADHILI UPASUAJI WA NGIRI MAJI (MABUSHA) RUFIJI

Jopo la Madaktari Bingwa 6 waongoza Kambi ya siku tatu ya upasuaji wa Ngiri Maji (Mabusha) kwa Zaidi ya wananchi 50 bila malipo katika Hospitali ya wilaya ya Utete chini ya ufadhili wa wawekezaji wa kilimo cha miwa na Kiwanda cha Sukari Rufiji (lake Agro). Meneja Rasimali watu kutoka Kampuni ya Lake Agro Innocent Mwaipopo

Jopo la Madaktari Bingwa 6 waongoza Kambi ya siku tatu ya upasuaji wa Ngiri Maji (Mabusha) kwa Zaidi ya wananchi 50 bila malipo katika Hospitali ya wilaya ya Utete chini ya ufadhili wa wawekezaji wa kilimo cha miwa na Kiwanda cha Sukari Rufiji (lake Agro).

Bwana Innocent Emmanuel Mwaipopo, Meneja Rasimali watu Lake Agro

Meneja Rasimali watu kutoka Kampuni ya Lake Agro Innocent Mwaipopo amesema ufadhili huo unagharimu zaidi ya milioni 60 ni sehemu ya kurejesha kwa wananchi wanaozunguka mradi huo walioshindwa kumudu gharama za matibabu ya upasuaji wa ngiri maji.

Aidha Bwana Mwaipopo amesema Lake Agro imekuwa ikifadhili huduma za kijamii ikiwemo ujenzi wa madarasa, Nyumba za Ibada na uchimbaji wa visima vya maji.

Wakieleza furaha yao, baadhi ya wananchi walionufaika na huduma, wamewasihi wananchi wengine wenye maradhi hayo kuondoa hofu na kujitokeza kupata huduma hiyo. Aidha Bwana Mwaipopo amesema Lake Agro imekuwa ikifadhili huduma za kijamii ikiwemo ujenzi wa madarasa, Nyumba za Ibada na uchimbaji wa visima vya maji.

Ally Byser, Daktari Bingwa wa Upasuaji njia ya Urolojia

Daktari Bingwa wa Upasuaji njia ya Urolojia (upasuaji na matatizo yanayoathiri mfumo wa mkojo, Figo, tezi za adrenal, ureta..) Ally Byser ametoa rai kwa jamii inayozunguka maziwa na mwambao wa pwani kuzingatia kinga zinazotolewa dhidi maradhi ya Ngiri Maji.

TAZAMA VIDEO HAPO CHINI

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »