NIRC MBIONI KUJENGA BWAWA LA UMWAGILIAJI SKIMU YA DAKAWA.

Mkuu wa wilaya ya Mvomero Mhe. Judith Nguli amewataka wanachama wa cha wakulima wa Ushirikawa Wakulima Wadogo Wadogo Kilimo cha Umwagiliaji Dakawa UWAWAKUDA katika skimu ya Dakawakuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali katika kuboresha sekta ya umwagiliaji nchini ikiwemoujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji na uendelezaji. Mhe. Judith Nguli ametoa kauli hiyo katika mkutano wa kawaida


Mkuu wa wilaya ya Mvomero Mhe. Judith Nguli amewataka wanachama wa cha wakulima wa Ushirika
wa Wakulima Wadogo Wadogo Kilimo cha Umwagiliaji Dakawa UWAWAKUDA katika skimu ya Dakawa
kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali katika kuboresha sekta ya umwagiliaji nchini ikiwemo
ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji na uendelezaji.


Mhe. Judith Nguli ametoa kauli hiyo katika mkutano wa kawaida wa mwaka wa chama cha ushirika
cha wakulima wa Umwagiliaji skimu ya Dakawa wilayani Mvomero mkoani Morogoro,ambapo
mkutano huo ulihudhuriwa na wataalamu wa Tume ya Taifa Umwagiliaji makao makuu,pamoja na
wataalamu ofisi ya Tume mkoa wa Morogoro.

Katika mkutano huo wataalamu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji wametumia wasaa huo kutoa elimu
ya umuhimu wa uchangiaji ada ya huduma za umwagiliaji na usajili wa chama cha umwagiliaji,
sambamba na kueleza mpango wa serikali katika kuendeleza eneo la umwagiliaji katika skimu ya
Dakawa.


“Moja kati ya vipengele ambavyo tunawaelimisha wakulima wetu waelewe kwamba miundombinu
iliyopo ni ya kwao lakini pia wachangie ili serikali iweze kufikia malengo yake, kwani kwa sasa eneo
linalofaa kwa umwagiliaji kwa nchi nzima ni hekta milioni 29 na eneo lililoendelezwa ni hekta 727,280,
hivyo serikali ina majukumu na wakulima wana wajibu wa kuchangia ili serikali iweze kuboresha
miundombinu iliyopo na kuiendeleza”


Kwa upande wake Mhandisi Umwagiliaji mkoa wa Morogoro Bw. Mohammed Mcheni, alibainisha
kuwa skimu ya Dakawa ni miongoni mwa skimu kubwa katika mkoa huo ambapo takribani bilioni 23.4
zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu hiyo ambapo uzalishaji wake ni zaidi ya gunia 20 kwa
ekari moja, hivyo serikali kuwekeza katika eneo hilo inaongeza usalama wa chakula kwa mkoa wa
Morogoro na Tanzania kwa ujumla.


“Eneo hili la Dakawa zipo hekta 1,000 ambazo hazijaendelezwa na zipo kwenye mpango wa mwaka
huu wa fedha kufanya upembuzi yakinifu wa kina pamoja na kufanyia usanifu na tutazijenga hizo
ambapo kukamika kwake kutakuwa na takribani hekari 8,000 ambazo zitatumika kwa ajili ya kilimo
cha umwagiliaji, kwahiyo serikali imedhamiria kuendeleza skimu ya Dakawa kwani ni eneo lenye
uwezo mkubwa wa kuzalisha chakula cha kutosha”


Naye, afisa sheria Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bi. Magreth Shayo, ametoa wito kwa wakulima wa
skimu ya Dakawa na wakulima wote nchini kuwa wakulima wapo katika mikono salama ya Tume ya
Taifa ya Umwagiliaji, kwani utekelezaji zoezi la uchangiaji ada ya huduma za umwagiliaji ni kwa mujibu
wa wa sheria na ina manufaa kwa wakulima hivyo itasaidia kukuza sekta ya umwagiliaji nchini.
VOX POPS WATAALAMU….

 1. Aidha wakulima wameishukuru Tume kwa kuwapatia elimu ya sheria ya taifa ya umwagiliaji kwani
  awali walikuwa na uelewa mdogo juu ya sheria ya taifa ya umwagiliaji inayomtaka mkulima kuchangia
  ada ya huduma za umwagiliaji na kusajili chama chini ya Tume ya Umwagiliaji, hivyo ujio wa wataalamu
  hao umewasaidia kuwa na uelewa wa umuhimu wa zoezi hilo kwa manufaa ya sekta ya umwagiliaji
  nchini.
 2. Skimu ya Dakawa ni skimu yenye ukubwa hekari 5016, ambapo serikali ipo mbioni kutekeleza mradi
 3. wa ujenzi bwala la umwagiliaji, ambalo litaongeza maji katika skimu hiyo ili kukabiliana na upungufu
 4. wa maji katika skimu hiyo na kuongeza uzalshaji wenye tija kwa
Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »