MSIBAMBIKIE WATU KESI ZA UONGO – CP HAMAD.

MSIBAMBIKIE WATU KESI ZA UONGO – CP HAMAD.

Kamishna wa Polisi Zanzibar CP. HAMAD KHAMIS HAMAD amewataka wananchi kuwacha tabia ya kutumia Vituo vya Polisi kushitaki kesi za uongo kwa lengo la kukomoana. Akikagua Mradi wa ujenzi wa Jengo jipya la Kituo cha polisi Mkoani, katika Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba ambacho kimegharimu Milioni mia saba, amesema wapo baadhi ya watu

Kamishna wa Polisi Zanzibar CP. HAMAD KHAMIS HAMAD amewataka wananchi kuwacha tabia ya kutumia Vituo vya Polisi kushitaki kesi za uongo kwa lengo la kukomoana.

Akikagua Mradi wa ujenzi wa Jengo jipya la Kituo cha polisi Mkoani, katika Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba ambacho kimegharimu Milioni mia saba, amesema wapo baadhi ya watu hutumia Askari wa Jeshi la Polisi wanaofahamu kufungua kesi za uongo na kesi za madai jambo ambalo ni kinyume na taratibu.

 Kwa upande wake Fundi Mkuu wa Ujenzi wa kituo hicho OMAR KHAMIS amesema wanatarajia kumaliza na kukikabidhi Kituo hicho baada ya wiki mbili zinazofuata.

Ujenzi wa Kituo cha Mkoani umekuja kufuatia kuchakaa kwa Kituo cha Polisi Mkoani ambacho kimerithiwa tokea wakati wa ukoloni na kinatumika hadi sasa.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »