DKT.MSONDE AMEWATAKA MAOFISA ELIMU KUKAMILISHA MIRADI YA ELIMU.

DKT.MSONDE AMEWATAKA MAOFISA ELIMU KUKAMILISHA MIRADI YA ELIMU.

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), anayeshughulikia Elimu, Dkt. Charles Msonde amewataka Maofisa Elimu nchini kusimamia miradi ya elimu kwa kufuata sheria, taratibu na miongozo na kutoruhusu vikwazo vya kukwamisha utendaji kazi wao. Akifunga kikao kazi cha Maofisa Elimu Mikoa na Wilaya kilichofanyika jijini Dodoma Oktoba 4,

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), anayeshughulikia Elimu, Dkt. Charles Msonde amewataka Maofisa Elimu nchini kusimamia miradi ya elimu kwa kufuata sheria, taratibu na miongozo na kutoruhusu vikwazo vya kukwamisha utendaji kazi wao.

Akifunga kikao kazi cha Maofisa Elimu Mikoa na Wilaya kilichofanyika jijini Dodoma Oktoba 4, 2023 Dkt. Msonde amesema ili miradi hiyo ikamilike inahitaji juhudi, uzalendo na uadilifu.

“Heshimu viongozi waliopo juu yenu lakini msiwaogope ili yale yanayoelekezwa na serikali yatekelezeke kwa kuwa lengo la hii miradi ni ya Lipa kulingana na matokeo hivyo kinachohitajika ni kuisimamia ikamilike kwa wakati kwa kuwa mahitaji ya kujenga shule za msingi na sekondari ni makubwa mno,”amesema Dkt.Msonde.

Amebainisha kuwa vipo vikwazo wanavyopitia Maofisa hao katika utekelezaji wa miradi hiyo lakini wasiache kusimamia sheria na taratibu ili ikamilike na kuanza kupokea wanafunzi ifikapo Januari 2024.

“Kuweni wajasiri simamieni sheria na taratibu zilizowekwa hakuna fedha zinazoletwa kwenye halmashauri bila mwongozo, mtu yeyote asikutoe kwenye reli simamia maelekezo bila kuangalia mtu,”amesema.

Kadhalika, ameagiza Maofisa hao kufanya tathmini ya miundombinu iliyokwama ikiwamo maboma yaliyojengwa na wananchi ili kupata gharama halisi zitakazosaidia serikali kutafuta fedha za kuikamilisha.

“Fanyeni tathmini kupata gharama sahihi na ndogo ambazo serikali ikipata fedha itaweza kugharamia, kwa mfano miradi ya EP4R, na majengo yaliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi,” amesema.

Awali, Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Elimu TAMISEMI, Vicent Kayombo, amesema katika kikao hicho wameangalia namna ya kuimarisha ubora wa elimu nchini na kutoka na maazimio 11 ikiwamo kuhakikisha wanafunzi wanamudu stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »