Unganisheni Nguvu Mshinde Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024.

Unganisheni Nguvu Mshinde Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Hemed Suleiman Abdulla amewataka Viongozi na wanachama wa CCM Mkoa wa Tanga kuunganisha nguvu zao na kuwa na lengo moja la kushinda kwa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika 2024. Akiwa katika muendelezo wa ziara yake ya kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi Wilaya

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Hemed Suleiman Abdulla amewataka Viongozi na wanachama wa CCM Mkoa wa Tanga kuunganisha nguvu zao na kuwa na lengo moja la kushinda kwa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika 2024.

Akiwa katika muendelezo wa ziara yake ya kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Pangani na Wilaya ya  Muhenza kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 amesema endapo Viongozi na  Wanachama wa CCM watakuwa wamoja katika kukitumikia, kukilinda na kutangaza mazuri yanayofanywa na CCM hakutakuwa na sababu itakayopelekea kukosa ushindi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa hata na Uchaguzi Mkuu ujao 2025.

Amefahamisha kuwa Mkoa wa Tanga umebahatika kuwa na Viongozi weledi na wachapa kazi ambao wamezidi kuimarisha mashirikiano  kati ya Chama na Serikali hatua ambayo inaashiriki kukipatia ushindi wa kishindo Chama cha Mapinduzi kwa nafasi zote kuanzia kata hadi Taifa.

Aidha amewasihi wale wote wanaotangaza nia ya kugombea nafasi mbali mbali za Uongozi katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 waache tabia hiyo na wasubiri wakati muafaka ufike ndipo watangaze nia zao kwani kufanya hivyo kwa sasa ni kukiuka kanuni na Sheria za Chama cha Mapinduzi

Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuulinda Muungano kwa juhudi zote ili uendelee kuwaunganisha Watanzania na yoyote atakaejaribu kuharibu taswira ya muungano huo atawajibishwa kwa mujibu wa Sheria.

Nae Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Ndg.  Rajab Abdulrahman Abdulla amemuhakikishia Mlezi wa CCM Mkoa wa Tanga kuwa ataisimamia vyema Miradi inayotekelezwa na Serikali kwa kuhakikisha inajengwa katika viwango vyenye ubora wa hali ya juu na kutoa onyo kwa wasimamizi wa miradi hiyo kuwa CCM Mkoa wa Tanga haitamvumilia yoyote atakaefanya ubadhirifu wa fedha na vifaa vya ujenzi wa  miradi hiyo.

Amefafanua kuwa kuwapatia maendeleo wananchi ndiko kunakowapelekea kuwa na imani na CCM na Serikali kwa ujumla hivyo, umakini na uwajibikaji kwa Viongozi wa ngazi zote za chama na serikali kutaleta matokeo chanya katika chaguzi zote nchini.

Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)
10 Oktoba, 2023

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »