RAIS DK.MWINYI AWATEMBELEA WAZEE.

RAIS DK.MWINYI AWATEMBELEA WAZEE.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi baada ya sala ya Ijumaa amewatembelea Wazee na kuwajulia hali wakiwemo Mjumbe wa Baraza la Ulamaa Mstaafu, Mwalimu Sheikh Machano Makame Machano nyumbani kwake Mwembe Makumbi Wilaya ya Mjini , Mkoa wa Mjini Magharibi . Pia alimtembelea Mzee Alawi Suleiman Khatib nyumbani kwake

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi baada ya sala ya Ijumaa amewatembelea Wazee na kuwajulia hali wakiwemo Mjumbe wa Baraza la Ulamaa Mstaafu, Mwalimu Sheikh Machano Makame Machano nyumbani kwake Mwembe Makumbi Wilaya ya Mjini , Mkoa wa Mjini Magharibi .

Pia alimtembelea Mzee Alawi Suleiman Khatib nyumbani kwake Makadara, Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi amejumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika ibada ya Sala ya Ijumaa viwanja vya Markas Bungi, Wilaya ya Kati Mkoa wa Mjini Magharibi.

Aidha Rais Dk.Mwinyi amesema kuamrishana mema na kukatazana mabaya ni jambo la msingi katika dini pia upande wa maisha ya dunia kwa Serikali kupitia watu ambao wanaamrishana mema wanasaidia kuleta amani, umoja, na utulivu nchini kwa maendeleo.

Vilevile amesema katika jamii kuna maovu mengi kunahitaji msaada wa kuyakataza na kuyakemea kupitia waumini na viongozi wa dini hususani kundi la vijana wanaojihusisha na mambo maovu katika kusema nao, kuwashajihisha waachane na vitendo hivyo waingie kumcha Mungu na kuwa na maadili mema.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »