RAIS DK.MWINYI ASEMA AMANI YA NCHI NI JAMBO LA MSINGI.

RAIS DK.MWINYI ASEMA AMANI YA NCHI NI JAMBO LA MSINGI.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi amewahimiza Waumini wa Dini ya Kiislamu kuendelea kuitunza amani na kudumisha umoja pamoja na mshikamano wa watu nchini. Rais Dk Mwinyi amesema hayo alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika Msikiti wa Masjid Kheir Batini

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi amewahimiza Waumini wa Dini ya Kiislamu kuendelea kuitunza amani na kudumisha umoja pamoja na mshikamano wa watu nchini.

Rais Dk Mwinyi amesema hayo alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika Msikiti wa Masjid Kheir Batini Nyamanzi, Wilaya ya Magharibi B Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 10 Novemba 2023.

Aidha Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa amani ya nchi ni jambo la msingi la kwanza.

Vilevile Rais Dk.Mwinyi ametoa pole kwa wananchi waliopata maafa kwa mvua zilizonyesha hivi karibuni, pia ni wajibu kumuomba Mwenyezi Mungu kwa mvua zenye neema.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »