Na.Elimu ya Afya kwa Umma, Ikiwa leo Novemba 17, 2023 Tanzania inaungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani, Rais Msataafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amezindua Mpango Harakishi wa Watoto Njiti na Watoto Wachanga. Akizungumza katika Uzinduzi huo Jijini Dar Es Salaam katika Mkutano wa Pili wa Kisayansi wa
Na.Elimu ya Afya kwa Umma,

Ikiwa leo Novemba 17, 2023 Tanzania inaungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani, Rais Msataafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amezindua Mpango Harakishi wa Watoto Njiti na Watoto Wachanga.
Akizungumza katika Uzinduzi huo Jijini Dar Es Salaam katika Mkutano wa Pili wa Kisayansi wa Afya ya Uzazi Mama na Mtoto Mhe.Kikwete amesema tatizo la kuzaliwa watoto njiti hapa nchini ni kubwa ambapo kuna takriban watoto wachanga
“Tatizo hili ni kubwa kuna takriban watoto wachanga mia mbili hamsini elfu huzaliwa Tanzania kabla ya wakati ni muhimu kuweka jitihada katika kupunguza hili”amesema Mhe. Kikwete.
Aidha, Mhe. Kikwete amesema Maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha kila Hospitali inatakiwa kuwa na Wodi maalum za Watoto njiti(NICU) hali itakayosaidia kuokoa maisha ya watoto .
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe amesema lengo la Serikali ni kuongeza kasi ya kupunguza vifo vya watoto wachanga ambapo ukiwa na kituo cha watoto wachanga inasaidia kupunguza vifo vya watoto wachanga kwa asilimia 50.