UTEKELEZAJI WA MPANGO JUMUISHI WA WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII.

UTEKELEZAJI WA MPANGO JUMUISHI WA WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII.

Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-TAMISEMI zimewakutanisha Wanganga Wakuu wa Mikoa Jijini Dodoma kutoka mikoa yote ya Tanzania bara lengo likiwa ni kujadili Utekelezaji wa Mpango Jumuishi na Endelevu wa kuwatumia Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii. Akizungumza katika Kikao hicho Mkurugenzi Huduma za Kinga,Wizara ya Afya Dkt. Ntuli Kapologwe amesema Wahudumu

Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-TAMISEMI zimewakutanisha Wanganga Wakuu wa Mikoa Jijini Dodoma kutoka mikoa yote ya Tanzania bara lengo likiwa ni kujadili Utekelezaji wa Mpango Jumuishi na Endelevu wa kuwatumia Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii.

Akizungumza katika Kikao hicho Mkurugenzi Huduma za Kinga,Wizara ya Afya Dkt. Ntuli Kapologwe amesema Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii wana Mchango mkubwa katika kukabiliana na masuala mbalimbali ya Afya ili kuleta mabadiliko chanya ngazi ya Jamii.

“Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii wanasaidia kuibua haraka viashiria mbalimbali vya magonjwa ngazi ya Jamii na kufikia haraka jamii katika maeneo wanayoishi”amesema.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, TAMISEMI Dkt. Wilson Mahera amesema katika kuhakikisha huduma ya afya Msingi inaimarika Mpango wa Serikali ni kuhakikisha Mifumo kwa Wahudmu wa Afya Ngazi ya Jamii inasomana ili kurahisisha utoaji wa Huduma za Afya.

Dkt.Mahera amebainisha hayo leo Novemba 22, 2023 Jijini Dodoma katika Kikao cha Waganga Wakuu wa Mikoa cha Kujadili utekelezaji wa Mpango Jumuishi na Endelevu wa Kutumia Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii.

“Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii ni muhimu kuzingatia kuhakikisha mifumo inasomana na mambo tunayojadili ni namna gani watawajibika na kila mhudumu mmoja ahudumu kaya 70 ikiwemo masuala ya lishe na mambo menhine ya afya”amesema.

Kwa Upande wake Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma Wizara ya Afya Dkt.Tumaini Haonga amesema kila mhudumu wa Afya ngazi ya Jamii atalipwa laki moja kwa mwezi ambapo kwa awamu hii Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii 28,000 wataanza huku mahitaji ni 137,294.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »