RAIS SAMIA ABARIKI CHONGOLO KUJIUZULU

RAIS SAMIA ABARIKI CHONGOLO KUJIUZULU

Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa kilichofanyika leo tarehe 29 Novemba, 2023 Jijini Dar es salaam na kuongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kimeridhia kujiuzulu kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho Comrade Daniel Chongolo Katibu wa

Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa kilichofanyika leo tarehe 29 Novemba, 2023 Jijini Dar es salaam na kuongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kimeridhia kujiuzulu kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho Comrade Daniel Chongolo

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi wa CCM Taifa, Paul Makonda amesema hayo leo Jijini Dar es salaam wakati akitoa taarifa kuhusu Kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kilichoketi leo Jijini Dar es salaam chini ya Mwenyekiti na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Pamoja na mambo mengine, kikao hicho kimejadili hali ya kisiasa ndani ya Chama na nje ya Chama hicho nchini na kimefanya uteuzi wa mwisho wa Wagombea wa nafasi za uongozi ndani ya Chama kwa ngazi ya Mkoa na Wilaya ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kifo na uteuzi wa nafasi nyingine.

Taarifa ya Katibu wa Itikadi na Uenezi na Mafunzo, Paul Makonda imeeleza walioteuliwa kugombea nafasi ya Uenyekiti kwa mikoa ya Arusha, Mbeya na Mwanza pamoja na Wilaya za Mpanda na Kusini Unguja.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »