BALOZI BYAKANWA AMETEMBELEA MABANDA YA WAJASIRIAMALI KUTOKA TANZANIA.

BALOZI BYAKANWA AMETEMBELEA MABANDA YA WAJASIRIAMALI KUTOKA TANZANIA.

Mhe. Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Mhe. Gelasius Byakanwa akiangalia bidhaa za wajasiriamali wa Tanzania alipowatembelea katika Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu Nguvu Kazi au Jua Kali yanayofanyika Viwanja vya Cercle Hyppique (Golf Course), Bujumbura, Burundi.  BALOZI wa Tanzania nchini Burundi, Mhe. Gelasius Byakanwa ametembelea

Mhe. Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Mhe. Gelasius Byakanwa akiangalia bidhaa za wajasiriamali wa Tanzania alipowatembelea katika Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu Nguvu Kazi au Jua Kali yanayofanyika Viwanja vya Cercle Hyppique (Golf Course), Bujumbura, Burundi. 

BALOZI wa Tanzania nchini Burundi, Mhe. Gelasius Byakanwa ametembelea mabanda ya Wajasiriamali wanaoshiriki Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu Nguvu Kazi au Jua Kali yanayoendelea kufanyika Bujumbura, Burundi.

Akiwa katika maonesho hayo, Balozi Byakanwa amewataka wajasiriamali kuendelea kufanya biashara zao kwa tija na ufanisi, pia amewahimiza kutumia fursa hiyo kutafuta masoko zaidi katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. 

Vili vile, ameipongeza Serikali kwa kuwezesha Wajasiriamali Wadogo na wa Kati kutoka maeneo mbalimbali nchini Tanzania kushiriki maonesho ambayo yanasaidia kukuza ajira na kupanua masoko ya bidhaa na huduma zao.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »