Mganga na mkewe wameuwawa kwa kukatwa katwa na shoka.

Mganga na mkewe wameuwawa kwa kukatwa katwa na shoka.

Mganga wa Tiba Asili ajulikanaye kwa jina la  Ngusa Jilumba (58)pamoja na Mkewe  Bugumba Mahola (54) wameuawa  papo hapo kwa  kukatwa na mapanga pamoja  na shoka baada ya kuvamiwa nyumbani kwao na watu wasiojulikana katika Kijiji cha Sungamile Halmashauri ya  Msalala Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga. Akizungumza  eneo la tukio  katika Kijiji hicho, Mwenyekiti wa Kijiji Cha Sungamile Charles Tungu amesema amezipata taarifa za

Mganga wa Tiba Asili ajulikanaye kwa jina la  Ngusa Jilumba (58)pamoja na Mkewe  Bugumba Mahola (54) wameuawa  papo hapo kwa  kukatwa na mapanga pamoja  na shoka baada ya kuvamiwa nyumbani kwao na watu wasiojulikana katika Kijiji cha Sungamile Halmashauri ya  Msalala Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.

Akizungumza  eneo la tukio  katika Kijiji hicho, Mwenyekiti wa Kijiji Cha Sungamile Charles Tungu amesema amezipata taarifa za mauaji hayo majira ya Saa nane Usiku Januari 20, 2023 ambapo Jeshi la Ulinzi Shirikishi(Sungusungu) walishirikiana.

“Baada ya kupokea taarifa za mauaji haya kwa kushirikiana na Jeshi la Ulinzi Shirikikishi(Sungusungu) na Jeshi la Polisi kupiga mwano walikuja na mapanga na walipitia shoka linalotumika kupasulia kuni wakalitelekeza shambani”amesema.

Aidha, ametoa wito kwa Wananchi wa Kijiji chake kuacha kujichukulia sheria mkononi huku akiomba Watalaam wa Kisaikolojia kuweza kuwasaidia msaada wa Kisaikolojia Watoto walioachwa na marehemu ikiwemo mlemavu wa macho aliyekatisha ndoto zake za kuendelea na elimu Chuo cha Serikali za Mtaa Hombolo kwani mara tu kumaliza kidato cha nne alipofuka.

Ester Juma ni  binti manusura  aliyeshuhudia Baba mkubwa na Mama mkubwa wakiuwa ndani ya nyumba hiyo  ambapo amesema yeye alikuwa amelala chumba kingine ambapo alisikia mlango ukipigwa na kitu kizito kasha kufunguliwa.

“Nilisikia mlango paa , mama mkubwa na Baba mkubwa wakapiga kelele, mara  nikasikia baba analia na kudondoka chini ,mama alijificha akajitokeza akasema tuna laki saba tunaomba tuwape , sauti ikasikika hiyo laki saba tunaweza kununua ng’ombe sisi  ??mama nikasikia tu mguu unakanyagwa paa  akaacha na kuongea sasa wakatoka , chumbani kwangu walinikuta baba mmoja hivi  na panga akanisonta  walikuja saa saba nikasikia nyumba ya pili kaka  asiyeona anapiga kelele   na iliyotumika ni shoka ya hapa waliitelekeza shambani sasa tunaogopa sijui tunaishije?amesema.

Watoto wa marehemu akiwemo Lukala Ngusa Jilumba wamesikitishwa kutokea kwa tukioa hilo huku wakiomba vyombo vya dola kuendelea kuchunguza zaidi ili kuwabaini waliofanya unyama huo.

“Nasikitika sana kwa wazazi wangu wawili kwa kufariki kwa siku moja kwa ajali mbaya ya namna hii ya kukatwakatwa na mapanga, mimi hapa nina changamoto ya kutoona na sioni naomba serikali ilifuatilie hili tukio maana mimi ni mlemavu wa macho tangu mwaka 2018 na wazazi wangu ndio nilikuwa nawategemea kwa kila kitu kama kuna uwezekano mimi nikasaidiwe nipate matibabu na tutaishije kwa unyama uliofanyika ni ngumu kuvumilia kwa sisi watoto”amesema.

Mzee Seni Jilumba ni kaka wa marehemu amesema hajawahi kusikia mgogoro wowote kwa marehemu huku jirani wa mji huo Masumbuko Doto amesema muda wa saa 7:45 usiku alitumiwa ujumbe wa maandishi kwenye simu ndipo walichukua hatua za kuchukua filimbi na kupiga mayowe ya sungusungu.

“Nilipokea ujumbe kuwa tumevamiwa na tukachukua hatua za haraka kupiga mayowe na tulipoanza ukaguzi tukakuta asubuhi shambani kuna bufa pamoja na shoka zimetupwa shambani ni tukio la kusikitisha tunaiomba serikali itujengee na kituo cha polisi hapa Sungamile”amesema.

Mtemi wa Jeshi la Ulinzi Shirikishi(Sungusungu) Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga Bundu Mswaki  Kahanya ameiomba Serikali kuongeza nguvu katika kulisaidia jeshi hilo ili kuimarisha ulinzi zaidi .

“Sisi huwa tunashirikiana sana na Serikali ila tunaiomba iongeze nguvu hasa vyombo vya dola kushirikiana na sisi mfano kupata vifaa vinavyoweza kunasa mapema watu wanaofanya vitendo kama hivi  tuungane nguvu maana wakati mwingine wahalifu wanakuwa na silaha nzito sisi hatuna namna”amesema.

Onesmo Daud ni Mtaalam wa Sheria  anasema watu waliopoteza maisha wamekoseshwa haki zao za msingi za kuishi .

“Mtu anayefanya mauaji anatakiwa apewe adhabu zake hivyo nasikitishwa na tukio hili naomba serikali iongeze nguvu ya kutosha, elimu ya haki za binadamu ili jamii ipate kuwa na uelewa kuhusu masuala mbalimbali ya haki ili kupunguza makosa jinai”amesema.

Marehemu wote wawili  Mke na Mme wamezikwa nyumbani kwao katika Kijiji cha Sungamile  Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga na waliuawa kwa kujeruhiwa kichwani na shingoni na kufa papo hapo kutokana na kuvuja damu nyingi huku mganga wa Tiba Asili Ngusa Jilumba akizikwa kwa kimila akiwa amekalishwa kwenye kaburi na tayari watu watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa upelelezi zaidi dhidi ya tukio hilo.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »