Watumishi wa Veta Pwani wasimamishwa kazi kwa kushindwa kusimamia ujenzi wa Chuo cha Veta mkoani humu

Watumishi wa Veta Pwani wasimamishwa kazi kwa kushindwa kusimamia ujenzi wa Chuo cha Veta mkoani humu

Na Barnabas Kisengi, Rufiji Januari 14 2021 WATUMISHI wawili wa Chuo chaVeta Pwani na kamati ya Manunuzi na ugavi yenye watu saba wamesimamishwa kazi mara baada ya kushindwa kusimamia vyema ujenzi wa Chuo cha Rufiji mkoani Pwani na kusababisha mradi kutokamilika kwa wakati. Uamuzi huo ulitolewa na  Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhandisi Omary

Na Barnabas Kisengi, Rufiji Januari 14 2021


WATUMISHI wawili wa Chuo chaVeta Pwani na kamati ya Manunuzi na ugavi yenye watu saba wamesimamishwa kazi mara baada ya kushindwa kusimamia vyema ujenzi wa Chuo cha Rufiji mkoani Pwani na kusababisha mradi kutokamilika kwa wakati. 
Uamuzi huo ulitolewa na  Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhandisi Omary Kipanga baada ya kutembelea mradi wa chuo hicho unaoendelea na kutokuridhishwa kabisa na utendaji kazi unaosimamiwa na Kamati hiyo ikiongozwa na msimamizi mkuu wa ujenzi Thomas Bwikizo pamoja na Afsa ugavi na mnunuzi Kubri Mkwanda. 

Mbali na umuamuzi huo alitoa siku tatu kwa  Makamu mkuu wa chuo cha VETA Pwani ambao ndiyo wahusika na wasimamizi wa mradi huo ,Clara Kibodya kuandika barua  ya kujieleza kwa nini hapaswi kusimamishwa kazi kutokana na mapungufu yaliyojitokeza na kutofanyia kazi.

Aidha Kipanga mara baada ya kukagua mradi huo na kuwahoji wasimamizi ilibainika kuwa kuna changamoto kubwa ya usimamizi mbovu na dalili za ubadhilifu wa pesa ambapo  walimkabidhi fundi mmoja majengo 16 tofauti na utaratibu ,ambapo aliiagiza TAKUKURU kufanya uchunguzi zaidi.

“Nyie wasimamizi kuanzia leo mnasimama kazi pamoja na hiyo kamati yenu ya watu saba kibaya zaidi mnampa mtu mmoja majengo 16 na hana uwezo wa kujenga majengo haya. tunaona kuna majengo mpaka sasa yako kwenye msingi na hayajamwagwa zege,kanuni na taratibu za  force account haziruhusu hivyo kuanzia sasa mtafuteni fundi mwingine na ndani ya miezi mitatu huu mradi uwe umekamilika “amesema kipanga
 “Serikali imewekeza kwenye hii miradi zaidi ya bilioni 40 zimepelekwa kwenye wilaya zote na iko kwenye ilani ya chama cha mapinduzi hivyo hatuko tayari kuona watu wachache wanatuharibia haiwezekani ,huu mradi ni mkubwa haikupaswa kupewa mtu mmoja ilipaswa kila jengo lipewe mtu mmoja hatupaswi kucheza na fedha za walipa kodi” amesema Kipanga. 


Alimtaka Mkurugenzi wa Veta ndani ya wiki moja kupata mrejesho na mpango kazi  kuhusu miradi miwili ya mafia na rufiji kujua kipi kimefanyika, mipango iliyopo na kujua hii kazi inakwisha lini.
Pia aliwaagiza Mkuu wa wilaya Luteni Kanali Patriki Savala pamoja na Mbunge wa Jimbo hilo Mohamed Mchengerwa kusaidia kupitia eneo hilo mara kwa mara kukagua ujenzi jambo ambalo litasaidia kukamilika kwa haraka.


Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo hilo Mohamed Mchengerwa amesema ujio wa Naibu waziri umekuwa na manufaa makubwa kutokana na maswali mengi anayoulizwa na wananchi wake kuhusu huo ujenzi uliochelewa kuanza kwani vijana wako mtaani bila ajira.
Ameomba Serikali kutoa miongozo ya ushirikishwaji kuanzia ngazi ya wilaya kwa ajili ya kushauriana na hata kushirikisha taasisi binafsi  ili kusaidia kusukuma suala hilo badala ya kuwaachia Veta peke yao na matokeo hawafanyi kazi kwa weledi. 

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »