Jeshi la Polisi wilayani Mafia laagizwa kumsaka na kumtia mbaroni Bwana Dickson Paul kwa kumiliki zahanati bila vibali

Jeshi la Polisi wilayani Mafia laagizwa kumsaka na kumtia mbaroni Bwana Dickson Paul kwa kumiliki zahanati bila vibali

Na Barnabas Kisengi, Mafia Januari 14, 2021 NAIBU Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Omary Juma Kipanga ameliagiza Jeshi la Polisi Wilaya ya Mafia Mkoani Pwani kumsaka na kumtia Mbaroni Bwana Dickson Paul mmiliki ambaye amefungua Zahanati bila kufuata Sheria na Taratibu zinazotakiwa. Kipanga ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Mafia ametoa agizo hilo

Na Barnabas Kisengi, Mafia Januari 14, 2021


NAIBU Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Omary Juma Kipanga ameliagiza Jeshi la Polisi Wilaya ya Mafia Mkoani Pwani kumsaka na kumtia Mbaroni Bwana Dickson Paul mmiliki ambaye amefungua Zahanati bila kufuata Sheria na Taratibu zinazotakiwa.


Kipanga ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Mafia ametoa agizo hilo Wilayani Mafia wakati alipokuwa kwenye ziara ya kikazi jimboni humo .
 Uamuzi huo ulikuja mara baada ya kupata malalamiko kutoka  kwa wananchi wa kijiji cha Chuguruma Kata ya Ndagoni Wilayani Mafia ambao walivamia msafara wake ili aweze kusikiliza kero zao ambapo Mh.Naibu waziri huyo alilazimika kuwasikiliza.
Wananchi hao walilamika kuwa hawapati huduma stahiki katika Zahanati ya Serikali iliyoko kijijini hapo na badala yake  uenda kupata huduma katika Zahanati iliyofungiliwa na Bwana Dcksoni katika Kitongoji cha Tumbuju ambeye ni mtumishi katika zahanati ya changuruma huku  kilicho mshangaza Naibu waziri kwani ndani ya Jimbo lake hana taarifa ya zahanati wala kituo cha afya ambacho kimejengwa wala kufunguliwa.

Mara baada ya kupata malalamiko hayo Mh.Naibu waziri alishangazwa na  taatifa  ya uwepo wa zahanati hiyo  ambaye yeye alikuwa halifahamu ndipo alipochukua hatua ya kufika katika eneo hilo ambalo zahanati hiyo inatoa huduma na  kubaini kuwa zahanati hiyo inamilikiwa na mtumishi Dickson Paul  anayefanya kazi katika zahanati ya kijiji hicho ambaye kwa sasa yuko Hospitali ya Muhimbili kimasomo kozi ya miezi sita inayohusiana na usingizi.
Mbali na kubaini mmiliki huyo lakini zahanati hiyo haiko kwenye mazingira mazuri ya kutoa huduma kwani iko kwenye makazi ya watu kama nyumba za wapangaji jambo ambalo lilimshangaza Naibu waziri kwani ni hatarii kwa jamii inayozunguka eneo hilo.
Aidha Kipanga alichukua jukumu la  kuwasiliana na mganga mkuu wa wilaya ya Mafia Daktari Zuberi Nzige na kufanya nae mazungumzo kwa njia ya simu kudhibitisha uwepo wa zahanati hiyo  ambaye na yeye alibainisha kuwa alishafika eneo hilo na kufanya ukaguzi na kukuta dawa za serikali  (msd) zikiwa zinatumika.
Maelezo aliyotoa mganga huyo Nzige  aliamuru zahanati hiyo ifungwe mara  moja huku akimtaka  bwana Dickson kufika kituoni kutoa maeleza na1 kukahidi agizo lake lakini cha kushangaza zahanati hiyo imekuwa ikitoa huduma kinyemela .

Hivyo basi mh.Naibu waziri baada ya kupata maelezo hayo alimtaka kamanda wa polisi Wilayani humo kumtafuta na kumkamata mhudumu wa zahanati hiyo  kutoa maelekezo ambaye alitoweka ghafla baada ya kupata taarifa za ujio wa Naibu waziri huyo huku akidai polisi  kumtafuta popote pale mmiliki wa zahanati ambaye anahatarisha maisha ya watu  ili kumfikisha kwenye vyombo vya kisheria .
Katika hatua nyingine aliwauliza viongozi wa mtaa wa eneo hilo ambapo walionekana kutokujua taarifa za mmiliki wa zahanati hiyo na wala hawakuwahi kumuita ofsini kwa ajili mahojiano zaidi jambo ambalo linaonyesha ni kiasi gani hawako makini na kazi zao.

“Inasikitisha yaani Mwenyekiti upo eneo hilo unaona Zahanati ikifunguliwa halafu haufatilii kujua kama ana leseni wala kibli na mhusika wa hapa haujui jina lake je kama kungetokea tatizo na madhara kwa wananchi nani  kulaumiwa?”alihoji Kipanga.
“Hapa inaonekana mmeshirikiana kabisa kila hatua haiwezekani usimjue maana vibali vinaanzia kwenu ngazi ya chini je kama ni majambazi mtafanyaje kiukweli hamuwatendei haki wananchi waliowachagua nahitaji ushirikiane na polisi kumtafuta mhusika huyu”amesema Naibu waziri Kipanga.
Pia katika hatua nyingine aliwataka wananchi kuhakikisha wanatoa taarifa kila jambo linalotokea kwenye kijiji kwa mamlaka husika ili kuweza kuepukana na utapeli unaoweza kujitokeza.


Aidha mwandishi wa habari wa Jfive Online  alichukua hatua ya kumtafuta mmiliki huyo Dickson Paul ambapo alipokea simu ya kiganjani na mara baada ya kutambilishwa anaongea na mwandishi wa habari na ili atoa ufafanuzi wa jambo hilo 
“Kiukweli mwandishi wa Habari hizo taarifa ninazona hiyo ni zahanati yangu lakini niko sehemu mbaya na hizo taarifa ni nzito sana nitakutafuta baada ya dakika tano ili nikae sehemu nzuri “Paul akieleza kwa njia ya simu.


Wananchi wakizungumza kwa nyakati tofauti walisema zahanati hiyo imekuwa hatarishi kwenye maisha yao kwa kutokuamini mhudumu huyo ambaye hana vigezo vya kutoa huduma hiyo kwani wapo ambao walipewa madawa na matokeo yake yakaleta madhara kwa kusokotwa na tumbo na mara wengine wanapokwenda kupata huduma hakuna ushirikiano wowote.

“Kuna Mwenzetu alifika kwenye hii zahanati mtoto akiwa mjamzito alipokelewa na kutelekezwa pale uchungu ulipoanza yule mhudumu akajifungia chumbani aligongewa mlango bila msaada na hatimaye wasamaria wema wakaingilia kati kumuokoa huyu mama na kujifungua mtoto njiti na baada ya muda mchache alifariki Dunia mtoto wake pengine ni kutokana na uzembe tunaomba mh.utusaidie ” alisema Sharifa akibubujikwa machozi.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »