Watumishi Mahakama kuu kanda ya Dodoma washerehekea wiki ya Sheria kwa kufanya Bonanza la Michezo.

Watumishi Mahakama kuu kanda ya Dodoma washerehekea wiki ya Sheria kwa kufanya Bonanza la Michezo.

Na Barnabas kisengi, Dodoma.January 30 2021 Mahakama kuu kanda ya Dodoma imeadhimisha siku ya sheria na miaka Mia moja tangu ianzishwe kwa kufanya bonanza la michezo mbalimbali katika uwanja wa jamuhuri kuelekea kilele cha siku ya sharia na miaka mia moja ya ya mahakama kuu ambayo kilele cha siku hiyo itakuwa February 01.2021 ambapo mgeni

Na Barnabas kisengi, Dodoma.January 30 2021


Mahakama kuu kanda ya Dodoma imeadhimisha siku ya sheria na miaka Mia moja tangu ianzishwe kwa kufanya bonanza la michezo mbalimbali katika uwanja wa jamuhuri kuelekea kilele cha siku ya sharia na miaka mia moja ya ya mahakama kuu ambayo kilele cha siku hiyo itakuwa February 01.2021 ambapo mgeni rasmi wa siku ya kilele hicho anatarajiwa kuwa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli 


Akizungumza katika bonanza hilo mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Denes Mpelambwa amesema katika wiki hii ya sheria mahakama kuu imeamua kufanya bonanza la michezo mbalimbali kwa kuwashirikisha watumishi wa mahakama kuu,mahakama za wilaya na mahakama za mwanzo kwa lengo la kufahamiana na kufanya mazoezi ili kujenga afya zao


“Tumeamua kufanya hivi ili watumishi wa mahakama wafaamiane na kufaya mazoezi haya watakuwa wamejea afya za mili yao kwani Sherehe hizi maranyingi hufanyikia dar es salaam lakini kwa mwaka huu sherehe hizi zimefanyika hapa makao mkuu ya serikali jijini Dodoma hivyo imetupa fursa mbalimbali za kufahamiana na watendaji wenzetu wa mahakama nyingine hapa nchini”amesema mpelembwa


Aidha mpelembwa amesema bonanza hili kwa kanda ya Dodoma litakuwa endelevu walau kila mwezi Wawe wanakutana walau mara moja badala ya kusubiri katika sherehe za sharia tu pia wakiwa wanatimiza miaka mia moja tangu kuanzishwa kwa mahakama kuu hapa nchini


“watumishi wenzangu mmeona faida ya kuwa na bonanza na kufanya mazoezi mara kwa mara kwani mnaiweka miili yenu vizuri na kuepuka na magonjwa mbalimbali hivyo sasa hakikisheni mnaendelea na kufanya mazoezi huko katika maeneo yenu mnakoishi na kushirikisha familia zenu kwani mazoezi hujenga afya ya mwili”

Kwa upande wao washiriki wa bonanza hilo ambao ni watumishi wa mahakama ambo wameshinda katika shindano la kula kwa mshindi wa kwanza na wapili Romani gandaweka na Winne kayombo wamefurahi kwa ushindi waliopata kwenye bonanza hilo huku wakiomba viongozi wa  mahakama kuhakikisha bonanza hilo linafanyika mara kwa mara ili waweze kujenga afya zao na kuepukana na magonjwa mbalimbali


Bonanza hilo lililoandaliwa na mahakama kuu lilihusisha mchezo ya kukimbi kuvuta kamba, mchezo wa rede mazoezi ya viongo, kukimbiza kuku na mashindano ya kula ambapo ushindi wa jumla umeongozwa na watumishi wa mahakama za mwanzo na washindi wa michezo mbalimbali wametunukiwa zawadi mbalimbalimbali na vyeti vya ushindi

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »