Wachukuliea hatua wote waliohusika kutoboa Bomba la mafuta yanayoshushwa kutoka kwenye meli” Mh. Kunenge.

Wachukuliea hatua wote waliohusika kutoboa Bomba la mafuta yanayoshushwa kutoka kwenye meli” Mh. Kunenge.

Kamati ya Usalama Mkoa wa Dar es salaam ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Aboubakar Kunenge ikiambatana na Watendaji wa Mamlaka ya Bandari na Wadau wa Kampuni za Mafuta leo February 03 wametembelea na kujionea uharibifu wa miundombinu ya kusafirisha Mafuta yanayoshushwa kwenye meli kwenda nchi kavu ambapo Mkuu wa Mkoa huo ametoa onyo

Kamati ya Usalama Mkoa wa Dar es salaam ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Aboubakar Kunenge ikiambatana na Watendaji wa Mamlaka ya Bandari na Wadau wa Kampuni za Mafuta leo February 03 wametembelea na kujionea uharibifu wa miundombinu ya kusafirisha Mafuta yanayoshushwa kwenye meli kwenda nchi kavu ambapo Mkuu wa Mkoa huo ametoa onyo kwa waliohusika kufanya uharibifu huo.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo RC Kunenge ameelekeza Kamati ya usalama Mkoa huo kuhakikisha wote waliohusika na hujuma hiyo wanakamatwa Mara moja na kuchukuliwa hatua Kali za kisheria kwakuwa kitendo walichofanya ni sawa na uhujumu uchumi.
RC Kunenge amesema kitendo Cha kutoboa Bomba hilo kinahatarisha usalama wa wananchi kwakuwa inaweza kusababisha Mlipuko lakini pia Mafuta yanayomwagika baharini yanaleta uchafuzi wa mazingira.
Aidha RC Kunenge amesema mbali na kuhatarisha usalama pia inasababisha Serikali kukosa Mapato, kusababisha uhaba wa Mafuta na pia kupoteza ubora wa Mafuta.
Pamoja na hayo RC Kunenge ameonyesha kuridhishwa na hatua zilizoanza kuchukuliwa na Mamlaka ya Bandari ikiwemo mchakato wa utaratibu wa manunuzi ya mfumo wa kuonyesha eneo lenye hitilafu na kutoa taarifa pamoja na kuimarisha ulinzi Katika eneo hilo.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa amesema wamejipanga kuhakikisha wanaanza msako wa pamoja na wanaamini watawatia mbaroni watu wote waliofanya hujuma hiyo.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »