Rais Dkt. Mwinyi leo amewaongoza wananchi katika mazishi ya Marehemu Dkt. Mohamed Seif Khatib kijijini kwao Umbuji, Mkoa wa Kusini Unguja.

Rais Dkt. Mwinyi leo amewaongoza wananchi katika mazishi ya Marehemu Dkt. Mohamed Seif Khatib kijijini kwao Umbuji, Mkoa wa Kusini Unguja.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi leo amewaongoza wananchi katika mazishi ya Marehemu Dk. Mohamed Seif Khatib yaliyofanyika huko kijijini kwao Umbuji, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja. Viongozi mbali mbali wa vyama vya siasa,dini na Serikali pamoja na wananchi walihudhuria katika mazishi hayo ambapo mapema

Inaweza kuwa picha ya Watu 7, watu wanasimama, watu wanakaa na ndani
Inaweza kuwa picha ya Watu 5, watu wanasimama na ndani
Inaweza kuwa picha ya Watu 4, watu wanasimama na nje
Inaweza kuwa picha ya Watu 2, watu wanasimama na nje

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi leo amewaongoza wananchi katika mazishi ya Marehemu Dk. Mohamed Seif Khatib yaliyofanyika huko kijijini kwao Umbuji, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.

Viongozi mbali mbali wa vyama vya siasa,dini na Serikali pamoja na wananchi walihudhuria katika mazishi hayo ambapo mapema Alhaj Dk. Mwinyi aliungana nao katika sala ya kumuombea Marehemu iliyosaliwa huko katika Masjidi Noor Muhammad (S.A.W), Mombasa kwa Mchina, Jijini Zanzibar.

Miongoni mwa viongozi waliohudhuria katika mazishi hayo ni Makamo wa Pili wa Rais Hemed Suleiman Abdulla, Rais wa Zanzibar Mstaafu wa Awamu ya Saba, Dk. Ali Mohamed Shein, Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mstaafu Balozi Seif Ali Idd pamoja na Viongozi wengine wa Serikali, viongozi wa CCM na vyama vyengine vya siasa.

Akisoma Wasifu wa Marehemu Dk. Mohamed Seif Khatib huko Umbuji, Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Khamis Abdalla Said alisema kuwa Marehemu amezaliwa tarehe 10 Januari 1951 huko kijijini kwao Umbuji, Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.

Alisema kuwa marehemu Mohamed Seif Khatib ambaye kifo chake kilichotokea jana (Februari 15,2021) huko katika Hospitali ya Al-rahma jijini Zanzibar baada ya kuugua kwa muda mfupi, Marehemu ameoa na kubahatika kuwa na watoto sita.

Alisema kuwa katika elimu, Marehemu alijiendeleza sana kielimu na kutunukiwa Shahada mbali mbali ikiwemo Shahada ya Ualimu ya Chuo cha Ualimu Nkrumah Zanzibar, Shahada ya Kwanza ya Elimu, Chuo Kikuu cha Dar-es Salaam, Shahada ya Uzamili katika Sanaa, London University SOAS na Shahada ya Uzamivu ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dodoma.

Katika uongozi wa Vijana, Naibu katibu Mkuu huyo alisema kuwa, Marehemu alianza uzoefu wa kazi kama Mwalimu wa Skuli mbali mbali akiwemo Mwalimu wa Skuli za Msingi, Mwalimu wa Skuli za Sekondari, Mkufunzi Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni Zanzibar pamoja na Mhadhiri wa muda, Chuo Kikuu cha Dodoma.

Kwa upande wa uongozi katika Wizara mbali mbali kuanzia mwaka 1988 hadi 2010, Marehemu aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Ofisi ya Makamu wa Rais anaeshughulikia Mambo ya Muungano, Waziri wa Mambo ya Ndani, Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo na Waziri wa Mambo ya Ndani, Ofisi ya Waziri Mkuu (Habari na Siasa).

Naibu Katibu Mkuu huyo akisoma Wasfu huo alieleza kwamba kwa upande wa uzoefu katika Siasa, Marehemu aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Uzini kuanzia mwaka 1988 hadi 2015, Mjumbe wa NEC, CCM kuanzia mwaka 1978 hadi mwaka 2017, Mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa CCM (Idara ya Siasa na Uenezi kuanzia mwaka 1995 hadi mwaka 20170.

Sambamba na hayo, kwa maelezo ya Naibu katibu Mkuu huyo, marehemu ameandika vitabu mbali mbali kama vile, Fungate ya Uhuru, Wasaka Tonge, Utenzi wa Ukombozi, Chanjo, Vifaru Weusi na Kipanga ambapo pia, ana miswada ambayo haijachapishwa.

Pia, alisema kuwa Marehemu amesimamia wanafunzi wa Uzamili na Uzamivu katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) na Chuo Kikuu cha Dodoma pamoja na kutunga nyimbo mbali mbali za taarabu na kuandika makala nyingi za Kiswahili.

Pamoja na hayo, Naibu Katibu Mkuu huyo alieleza kwamba Marehemu vile vile alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili Zanzibar kuanzia mwaka 2014 hadi kufariki kwake lakini pia, alikuwa Mjumbe wa Kamisheni ya Utumishi Serikali.

Katika wasfu huo pia, Naibu Katibu Mkuu huyo alisema kuwa Marehemu alikuwa ni miongoni mwa wanafunzi wa mwanzo waliochukua Uzamivu (PhD ya Kiswahili) hapa nchini.

Halikadhalika, Wasfu huo ulieleza kwamba Marehemu Dk. Mohamed Seif Khatib ameacha athari kubwa kwenye lugha ya Kiswahili. Inalilahi waina ilaihi Rajiun, Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mahala pema peponi, Amin

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »