DKT, DUGANGE AKERWA NA USIMAMIZI MBOVU KITUO CHA AFYA KATA YA WANGING’OMBE ATOA SIKU 30.

DKT, DUGANGE AKERWA NA USIMAMIZI MBOVU KITUO CHA AFYA KATA YA WANGING’OMBE ATOA SIKU 30.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt Festo Dugange (MB) ametoa muda wa siku 30 kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe Mkoani Njombe kuhakikisha wanafanya maboresho ya utoaji huduma katika Kituo cha Afya Kata ya Wanging’ombe. Februari 15/2021 akiwa kwenye ziara ya kikazi Jimboni Kukagua utekelezaji wa miradi ya Maendeleo na kusikiliza kero

Inaweza kuwa picha ya Watu 2, watu wanakaa na nje
Inaweza kuwa picha ya Watu 3, watu wanakaa na nyasi
Inaweza kuwa picha ya Mtu 1, amesimama, nyasi na mti

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt Festo Dugange (MB) ametoa muda wa siku 30 kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe Mkoani Njombe kuhakikisha wanafanya maboresho ya utoaji huduma katika Kituo cha Afya Kata ya Wanging’ombe.

Februari 15/2021 akiwa kwenye ziara ya kikazi Jimboni Kukagua utekelezaji wa miradi ya Maendeleo na kusikiliza kero za Wananchi Dkt, Dugange alisema maboresho hayo yaende sambamba na kuimarisha mfumo mzima wa Uongozi unaosimamia huduma za Afya Kituoni hapo.

Dkt, Festo Dugange aliwasili kituoni hapo kwa lengo la kubaini uhalisia wa malalamiko ya Wananchi juu ya ukosefu wa dawa katika kituo hicho na baada ya kufanya ukaguzi alibaini kuwa Kituo hicho kimekosa dawa muhimu ikiwemo Amoxicillin kwa zaidi ya miezi minne iliyopita huku Wagonjwa wakilazimika kwenda kununua nje ya Kituo.

“Yapo mambo hayaendi sawa hapa yaani Dawa zinanunuliwa, mtoaji na mpokeaji wa Dawa Kituoni kisha kupeleka kwa Wagonjwa ni mtu mmoja inamaana hapa kuna upotevu Mkubwa wa dawa pia hakuna kabisa matumizi ya Ishu vocha hata Takwimu za Wagonjwa na matumizi ya dawa hakuna” Dkt, Dugange.

Baadhi ya Wananchi wa Kata ya Wanging’ombe akiwemo Greyson Mahwata na Agness Mgina walikiri uwepo wa changamoto ya ukosefu wa dawa kwa kipindi cha muda mrefu hali ambayo iliwalazimu kununua dawa katika Maduka ya dawa yaliyopo mitaani kwa gharama kubwa.

Diwani wa Kata ya Wanging’ombe Geofrey Nyagawa alisema baada ya Ziara ya Naibu Waziri anatarajia kuona mabadiliko makubwa Kituoni hapo kwakuwa anaamini utekelezaji wa maagizo hayo utaanza maramoja Ili adhma ya kuwahudumia Wananchi iweze kutimia.

Miradi mbalimbali imetembelewa na Mhe, Naibu Waziri TAMISEMI Dkt, Festo Dugange ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Wanging’ombe pia ukaguzi wa Miradi mingine unaendelea katika Kata zote za Jimbo hilo.

OR-TAMISEMI, NJOMBE

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »