Serikali ya Tanzania na Burundi zimekutana mkoani Kigoma kujadili namna nchi hizo mbili zinavyoweza kushirikiana katika sekta ya madini ili kukuza uchumi wa nchi kwa pamoja kupitia rasilimali hiyo . Kikao hicho kimehusisha balozi wa Tanzania nchini Burundi Dr Jilly Maleko na Balozi mdogo wa Burundi nchini Tanzania Kabura Cyriaque pamoja na watalamu wa madini
Serikali ya Tanzania na Burundi zimekutana mkoani Kigoma kujadili namna nchi hizo mbili zinavyoweza kushirikiana katika sekta ya madini ili kukuza uchumi wa nchi kwa pamoja kupitia rasilimali hiyo .
Kikao hicho kimehusisha balozi wa Tanzania nchini Burundi Dr Jilly Maleko na Balozi mdogo wa Burundi nchini Tanzania Kabura Cyriaque pamoja na watalamu wa madini wa pande zote mbili ambapo unalenga kuja na makubaliano ya pamoja ya jinsi nchi hizi zitakavyotumia rasilimali ya madini .
Akiongea kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Kigoma ,kaimu katibu tawala mipango na uratibu Samuel Tenga amesema hatua hiyo itatoa fursa ya kibiashara na ajira kwa wananchi.
Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *