Kanisa la Moravian Mabibo lajipanga Kuwafikia watu wenye Uhitaji.

Kanisa la Moravian Mabibo lajipanga Kuwafikia watu wenye Uhitaji.

Na; Emesto Eliudy, Dar ES Salaam Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Mashariki Ushirika wa Mabibo kupitia Idara ya Ustawi wa Jamii, limejipanga kuwafikia watu mbalimbali wenye uhitaji wakiwemo Yatima, Wajane na Wazee ambao wanaishi katika mazingira yasiyo Rafiki. Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar Es Salaam na Mratibu wa Idara hiyo, Bi Editha Albert wakati wa

Mratibu wa Idara ya Ustawi wa Jamii Ushirika wa Mabibo, Bi. Editha Albert

Na; Emesto Eliudy, Dar ES Salaam

Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Mashariki Ushirika wa Mabibo kupitia Idara ya Ustawi wa Jamii, limejipanga kuwafikia watu mbalimbali wenye uhitaji wakiwemo Yatima, Wajane na Wazee ambao wanaishi katika mazingira yasiyo Rafiki.

Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar Es Salaam na Mratibu wa Idara hiyo, Bi Editha Albert wakati wa Ibada ya Sikukuu ya Ustawi wa jamii iliyofanyika Katika Kanisa la Moravian Ushirika wa Mabibo ambapo alisema kuwa Idara hiyo imejipanga kuwafikia watu wengi Zaidi ambao wanaishi maeneo ya jirani na Kanisa hilo bila kujali wanatoka Dini gani.

“Tumekuwa tunafanya huduma mbalimbali kwa Habari ya mahitaji na huduma za kiroho. Mwaka jana kanisa lilitoa kiasi cha Tsh. Milioni nne (4) kwa ajili ya huduma kwa makundi ya watu wenye uhitaji ambao walikuwa ni watu wanaosali kanisani tu. Lakini kwa mwaka huu  Idara inatamani kuwafikia watu wengi Zaidi wenye uhitaji ambao wanakaa maeneo ya Jirani na Kanisa Bila kujali wanatokea katika Dini gani. Alisema Bi. Editha.

Aidha Bi Editha aliongeza kwa kusema kuwa, awamu hii Idara hiyo imejipanga kukamilisha ujenzi wa nyumba ya mama Mjane ambayo imefikia hatua ya kupauliwa.

“Pia Mwaka huu idara tutakamilisha ujenzi wa nyumba ya mama mjane ambayo imefikia kwenye hatua za mwisho, tunaamini kwamba tukifanya hivi tutakuwa tumeokoa familia ya Mjane  huyu na watu wengine lakini pia utakuwa ni ushuhuda kwa kanisa kwamba tumeweza kuhudumia watu wa aina hii kwa kuwapatia makazi salama. Alisema Bi. Editha.

Kwa upande wake Mchungaji wa Jimbo la Mashariki ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wilaya ya Kusini Mch. Bwigane Mwakalinga amaelipongeza Kanisa La Moraviani kwa kuweka utaratibu maalumu wa namna ya  kuwasidia watu wenye Uhitaji kwenye jamii na kuwashukuru waumini wa kanisa hilo kwa Sadaka zao wanazozitoa kwa ajili ya kuwategemeza wajane, yatima na wahitaji wengine wenye makundi toafuti.

Mchungaji wa Jimbo la Mashariki ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wilaya ya Kusini Mch. Bwigane Mwakalinga

“Hakuna jamii ambayo haina wahitaji, jamii yoyote ile ina wahitaji na Kwakuwa ina wahitaji tunawajibika kama kanisa Kwa kuwatunza na kuwaona wahitaji katika Dhiki zao kama ambavyo mtumishi wa Mungu Yakobo  anavyotuasa katika kitabu chake anapotuambia kuwa Dini iliyosafi ni kuwatazama yatima na wajane katika dhiki zao.Tunawashukuru waumini wa Kanisa la Moravian kwa kuguswa na kutoa Sadaka zao kwa ajili ya wahitaji. Alisema Mchungaji Bwigane

Pia Mch. Bwigane aliwataka Watanzania Kuwasaidia watu wenye Uhitaji  kwa Mioyo ya ukarimu kwani hakuna aliyefika mahali alipo bila kupewa msaada.

Nikuombe ewe Mtanzania sio lazima uwe Mkristo  wa dini yoyote ile angalia pembeni yako mhitaji aliyeko msaidie  kwa moyo wa ukarimu kabisa kwa sababu Mungu aliyekubariki wewe anajua kabisa amekubariki  kwa ajili ya kuwasaidia Wengine, nina amini kabisa wewe ambaye utamsaidia mhitaji na wewe kuna sehemu ulisaidiwa  ukawa mahali ulipo. Alisema Mch. Bwigane

Kanisa la Moravin limeweka utaratibu wa kuwa na Ibada ya Ustawi wa jamii ambayo hufanyika mara moja kwa mwaka ifikapo mwezi wa pili yenye lengo la kukusanya fedha na misaada mbalimbali inayoelekezwa kwa watu wenye uhitaji ambao ni Wajane na Yatima Pamoja na wazee wanaoishi katika mazingira Hatarishi.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »