Katika kuelekea kilele cha sikukuu ya wanawake duniani ambayo huadhimishwa March 8, mwaka huu Serikali imesema sikukuu hizo zitaadhimishwa kwa ngazi ya mikoa ambapo kumekuwa na Kongamano lililojumuisha wanawake wa Mkoa wa Geita lililoandaliwa na FETTYFIVE kwa kushirikiana na WAG HILL lililoafanyika leo tarehe 6/3/2021 Katoro katika ukumbi wa JJ Hotel. Katika Kongamano hilo mgeni
Katika kuelekea kilele cha sikukuu ya wanawake duniani ambayo huadhimishwa March 8, mwaka huu Serikali imesema sikukuu hizo zitaadhimishwa kwa ngazi ya mikoa ambapo kumekuwa na Kongamano lililojumuisha wanawake wa Mkoa wa Geita lililoandaliwa na FETTYFIVE kwa kushirikiana na WAG HILL lililoafanyika leo tarehe 6/3/2021 Katoro katika ukumbi wa JJ Hotel.
Katika Kongamano hilo mgeni RASMI alikuwa KATIBU CCM WILAYA YA MBOGWE Ndg GRACE SHINDIKA ambaye aliwakumbusha Wanawake kuachana na dhana potofu kama mila na desturi zinazomwona Mwanaume pekee ndiyo anaefaa kuwa Kiongozi, Mfumo DUME katika jamii kuwa Mwanamme ni Kichwa,Rushwa ya Ngono katika kujitokeza Kugombea nafasi za Uongozi .
Shindika ameendelea Kuwaasa kinamama kuielimisha jamii juu ya hayo na kuwaomba Wanawake kuendelea kutoa elimu bora kwa watoto ambao ni taifa la kesho
Aidha shindika amewaasa wanawake kuhakikisha wanakuwa wajasili na kujitokeza katika nafasi mbalimbali za uongozi katika maeneo mbalimbali Kama taasisi binafsi, taasisi za dini serikalini na kwaenye vyama vya siasa kwani wanawake wakipata nafasi wanaweza na wanahofu ya mungu na wanawake ni wazalendo
Na Barnabas Kisengi
Geita March 6, 2021
Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *