WAZIRI WA AFYA DKT. DOROTHY GWAJIMA APOKEA VIFAA VYA MICHEZO

WAZIRI WA AFYA DKT. DOROTHY GWAJIMA APOKEA VIFAA VYA MICHEZO

Na Mwandishi wetu-Dar es Salaam Duka la vifaa vya michezo la Just Fit imemkabidhi vifaa vya vya mazoezi kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima, kuunga mkono juhudi zake na Wizara hiyo anayoiongoza katika kuhamasisha jamii kufanya mazoezi ya viungo. Hafla hiyo imefanyika leo Dar es Salaam, eneo

Na Mwandishi wetu-Dar es Salaam


Duka la vifaa vya michezo la Just Fit imemkabidhi vifaa vya vya mazoezi kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima, kuunga mkono juhudi zake na Wizara hiyo anayoiongoza katika kuhamasisha jamii kufanya mazoezi ya viungo.


Hafla hiyo imefanyika leo Dar es Salaam, eneo la Mlimani City lilipo duka hilo, ambapo Dk. Gwajima ametumia nafasi hiyo kueleza mpango wa Serikali wa kuandaa Mwongozo Maalum wa jinsi ya kufanya mazoezi sambamba na lishe inayofaa, utakaosimamiwa na Maofisa Michezo wa Mikoa na Wilaya, watakaoelimisha jamii juu ya mazoezi sambamba na lishe bora.

“Ninashukuru kunialika hapa leo, nilipata salamu kupitia Ofisa Habari wangu baada ya shughuli za mazoezi Mimi na familia pamoja na Wizara yangu, mmekuwa mkifuatilia na mkaona mtuunge mkono katika hili.
“Nawapongeza kwa sababu maduka yapo mengi lakini ninyi mmeona mniunge mkono na mnipongeze kwa hiyo nikaona ni heshima kubwa, nije kwa sababu hili ni suala la kijamii, la wadau wengi kutiana moyo ikizingatiwa kwamba walio wengi katika nchi zinazoendelea hatukuwezeka katika kufanya vizazi vyetu vipende mazoezi,” alisema.


Dk. Gwajima aliongeza “Kwa hiyo kadri tunavyozidi kwenda kwenye tasnia ya afya, siyo tu Tanzania bali duniani kote, tunaanza kuona tunapata ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza ambayo matibabu yake ni  gharama kubwa sana lakini ukiangalia asili ya magonjwa haya ni kwa sababu tumeacha kufanya mazoezi.
Amesema mazoezi ni asili ya viungo vyote, hata hivyo sisi tumeacha tumeingia katika mfumo wa kuzuia miili yetu kutokwa jasho, kufanya mazoezi.
“Tumeacha  magonjwa hayo yakapata  fursa ikiwamo kisukari, shinikizo la damu, moyo na mengine kama hayo, imekuwa ikielezwa na wanasayansi na wala si siri kwamba magonjwa haya tunaweza tukarudisha chini kasi yake ama kuyaondosha kabisa kama tutazingatia mazoezi na lishe iliyo bora.
“Sasa huwezi kuongelea lishe bora kama hujafanya mazoezi hupata matokeo yaliyo bora, sasa tufanyaje?.. lazima sisi tuliopo kwenye umri huu, tumesoma, tumefikia hapa, tupambane na magonjwa haya , tuwekeze nguvu nyingi kuwa wa mfano kuhakikisha kizazi kijacho kije kikute tulijiandaa vizuri,” Alisema.


Amesema yeye Waziri wa Afya peke yake hawezi na kwamba hakuna Wizara yoyote Tanzania inayoweza bila wadau mbalimbali kuja kuipokea hii dhana na kuitangaza.
Amesema mazoezi yana aina yake ya kufanya, huwezi kufanya mazoezi umevaa kitenge,kuna mambo ya kuzingatia kuanzia nguo ambazo mtu anavaa lazima zimuache huru na viatu anavyovaa kwani asipozingatia anaweza kuvaa viatu visivyofaa na kuishia kupata maumivu.
“Kwa hiyo lazima tueleweshe wananchi hizi ni zama za mazoezi, kama unataka kuishi vizuri uchumi wako na muda wako uelekeze kwenye kujitafutia afya anza na mazoezi,” alisisitiza.
Aliongeza “Mazoezi yapo ya aina nyingi kulingana na umri na afya ya mtu, wembamba nao wanapata kisukari, kuna sababu zake nao, kupitia mwongozo wataelimishwa aina ya mazoezi ya kufanya, na lishe, kadhalika wale waliozidi uzito nao wataelimishwa mazoezi gani na lishe ipi ya kuzingatia.
“Mfumo wa mazoezi ukienda vizuri, mfumo wa damu ukakaa sawa, mzunguko wa damu na hewa na chakula kikapokewa vizuri, kikafyonzwa vizuri magonjwa mengi utaachana nayo.
“Hata yakija yatakutembelea katika kukuimarisha hutalala sana, ukatumia muda na dawa nyingi Sana, mwisho ukakorofisha figo na maini.
“Kwa hiyo, nimekuja hapa kwa heshima hiyo, nitumie fursa hii ukishafanya mazoezi na lishe yako vizuri bila kusahau tiba asili ambayo tunaielezea kila saa, chukulia zile jamii za vijijini wanavyokula vyakula vya mimea na  juisi na dawa zao, ukiangalia wanavyougua utaona dhairi ni tofauti na sisi wa mijini, tunaokula kisasa” alisema.


Amesema lakini vyakula peke yake havitoshi bila kuzingatia mazoezi na mazoezi lazima mtu ajiandae kuyafanya rafiki usije ukayachukia.
“Ukavaa viatu ukachubua, ukavaa nguo ukapata matatizo itakuwa si sawa, niwaombe wauzaji wa vitu vya michezo mjipambanue, mmeniambia mpo Arusha, Dar es Salamm na mnakuja Dodoma.
“Nawapongeza siku ya wanawake mlishusha bidhaa kwa asilimia 50, ili wasio na uwezo wanaotaka kufanya mazoezi nao wapate tumaini kwamba mazoezi si biashara ya matajiri ni ya kila mtu.

“Nimefurahi mna nguo mpaka za watoto,nashauri mazoezi yaanzie mpaka utotoni, familia zifanye mazoezi ndiyo tuwarithishe watoto urithi nzuri wa afya na si magari mengi, Ila urithi wa afya haupo. akiumwa mmoja kwenye familia vyote mtaviuza vitapotea, huo unakuwa si uendelevu,” alisema.
Waziri huyo aliahidi kufanya kikao na wenye maduka waeleweshe  Dhana ya kuvaa vizuri wakati wa mazoezi Ina faida gani na elimu hiyo ifike hadi vijijini.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »