Imeelezwa kuwa Wanawake zaidi ya asilimia 50% wanategemea ardhi kwaajili ya kipato chao.

Imeelezwa kuwa Wanawake zaidi ya asilimia 50% wanategemea ardhi kwaajili ya kipato chao.

Na.Saleh Ramadhani. DODOMA. Kamishna ustawi wa jamii Dokta Naftali Ng’ondi amebainisha kuwa wanawake zaidi ya asilimia 50% wanategemea ardhi kwajili ya kipato chao.kauli hiyo imetolewa jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano uliokuwa ukifanyika kwa njia ya mtandao ambao umehusisha nchi wanachama wa UN zaidi ya 140. Dkt Naftali ameeleza kuwa uelewa na muamko wa wakina mama

Na.Saleh Ramadhani. DODOMA.

Kamishna ustawi wa jamii Dokta Naftali Ng’ondi amebainisha kuwa wanawake zaidi ya asilimia 50% wanategemea ardhi kwajili ya kipato chao.kauli hiyo imetolewa jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano uliokuwa ukifanyika kwa njia ya mtandao ambao umehusisha nchi wanachama wa UN zaidi ya 140.

Dkt Naftali ameeleza kuwa uelewa na muamko wa wakina mama wa kumiliki ardhi bado ni mdogo katika nchi ya Tanzania huku akisema Serikali imeweka mkakati madhubuti wa kuweza kuhamasisha wakina mama kutambua umuhimu wakuwa na ardhi pamoja na kuimiliki ardhi ambapo kaongeza  kuwa ’katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatamka wazi kuwa kila mwananchi ana haki ya kumiliki ardhi bila kujali jinsia yake akiwa na maana ya kuwa wanawake na wanaume wana haki hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa LANDESA Monica Muhoji amesema LANDESA ni shirika ambalo limejikita katika masuala ya haki ya ardhi na mambo mengine yote yanayoendana na masuala ya ardhi huku wakiangalia usalama wa wananchi hususani kwa wanyonge au watu ambao wameachwa katika nafasi zao kwa njia mbalimbali kama vile wanawake,Vijana,Wazee watu wenye ulemavu na makundi kama ya wafugaji.

Naye Mboni Mgaza kaimu mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Jinsia chini ya Wizara ya Afya Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii amesema Wizara pamoja na majukumu mengine imepewa jukumu la kusimamia utekelezaji wa sera ya wanawake na jinsia.

IMkutano huo hufanyika kila mwaka ambao hutoa fursa kwa wataalamu wanaohusika na afua mbalimbali za utekelezaji kwaajili ya kuleta usawa wa kijinsia na kujadiliana juu ya mafaniko ambayo yamepatikana katika.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »