UVCCM TAIFA WAMPONGEZA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

UVCCM TAIFA WAMPONGEZA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

Na Saleh Ramadhani.DODOMA. UMOJA wa vijana wa chama cha Mapinduzi CCM Taifa umempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Hassani Suluhu kwa kupata nafasi ya kuliongoza taifa la Tanzania.  Hayo yamebainishwa leo jijini Dodoma na Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Herry James wakati akizungumza na waandishi

Na Saleh Ramadhani.DODOMA.

UMOJA wa vijana wa chama cha Mapinduzi CCM Taifa umempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Hassani Suluhu kwa kupata nafasi ya kuliongoza taifa la Tanzania. 

Hayo yamebainishwa leo jijini Dodoma na Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Herry James wakati akizungumza na waandishi wa habari katika kikao kilichofanyika katika ofisi za chama hicho.

umoja wa chama hicho unampongeza Rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania Samia Hassani Suluhu kwa kupata nafasi hiyo na kuahidi kumuunga mkono katika kutekeleza majukumu yake ya kujenga taifa.

“Kwanza kabisa niungane na viongozi wa chama cha Mapinduzi CCM, viongozi wa Serikali na vijana wa chama cha Mapinduzi na vijana wote nchini kutoa pole kwa familia ya hayati John Pombe Magufuli aliyekuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,mama Samia Suluhu na watanzania kwa ujumla kwa msiba mzito tulioupata wa kumpoteza mtanzania Mzalendo hayati Dkt John Pombe Magufuli mwenye kujali maslahi ya Tanzania lakini pia tunampongeza rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mh Samia Hassani Suluhu kwa kupata nafasi hii ya kuiongoza nchi”. Amesema Herry James

Sambamba na hilo amesema kuwa wapo tayari kumuunga mkono rais wa sasa mh Samia hassani Suluhu katika kufanya yale yenye kuleta maendeleo kwa ajili ya kujenga taifa. 

“kwa matakwa ya katiba ya Tanzania tumempata rais wetu mpya mh Samia Hassani Suluhu ambae ndiye atatuongoza katika kujenga nchi ya Tanzania, tunaahidi kumuunga mkono na kumpa ushirikiano wa hali na Mali katika kuhakikisha dhamira yake njema ya kulijenga taifa inafanikiwa kwa asilimia zote”amesisitiza Herry

Licha ya hilo Herry amesema kuwa katika hotuba iliyotolewa na rais Samia Suluhu Hassani wakati anaapishwa alisisitiza kuyaacha yaliyopita na kuganga mapya kwa maslahi ya taifa hivyo kuyafuata maneno hayo ili kujenga nchi ya Tanzania.

“wakati Rais Samia Suluhu Hassani anaapishwa alitoa hotuba yenye kuleta dira ya wapi nchi yetu inaelekea na alisisitiza kama taifa kushikana mikono kwa pamoja na kuyaacha yaliyopita na kuganga mapya kwa ajili ya kujenga taifa ambalo linahitaji nguvu zetu kama watanzania’’amesema Herry.

Pia Herry amesisitiza kwa kuwatoa mashaka vijana wa chama cha mapinduzi na vijana wa Tanzania kumpa ushirikiano Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kumrahisishia katika kuyatekeleza yale yaliokusudiwa kwa manufaa ya taifa la Tanzania.

‘‘Yale yaliokusudiwa kufanyika kwa ajili ya vijana wa Tanzania naamini yataendelea kutekelezwa kwa kuwa rais Samia Hassani Suluhu alikuwa ni kiongozi wa karibu na hayati Dkt John Pombe Magufuli hivyo anafahamu ni yapi yaliyokusudiwa kufanywa kwa vijana na atayatendea haki hivyo niwasisitize vijana wa chama cha Mapinduzi na taifa kwa ujumla kumuunga mkono na kuwa na dhamira kama ya mh rais ili kuendana na kasi yake ya maendeleo’’.Amesisitiza Herry

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »