Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa Mwaka ulioishia Mwezi April Mwaka huu 2021umeongezeka kwa Asilimia 3.3.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa Mwaka ulioishia Mwezi April Mwaka huu 2021umeongezeka kwa Asilimia 3.3.

MFUMUKO wa Bei wa Taifa kwa Mwaka ulioishia Mwezi April Mwaka huu umeongezeka hadi kufikia Asilimia 3.3 kutoka asilimia 3.2kwa Mwaka ulioishia Mwezi Machi Mwaka huu ambapo imechangiwa na kuongezeka kwa bei za bidhaa za vyakula. Hayo yameelezwa hii leo Jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi  Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Ruth Minja wakati

Nafaka.

MFUMUKO wa Bei wa Taifa kwa Mwaka ulioishia Mwezi April Mwaka huu umeongezeka hadi kufikia Asilimia 3.3 kutoka asilimia 3.2kwa Mwaka ulioishia Mwezi Machi Mwaka huu ambapo imechangiwa na kuongezeka kwa bei za bidhaa za vyakula.

Hayo yameelezwa hii leo Jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi  Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Ruth Minja wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari ambapo amesema kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi April 2021 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Machi 2021.

Aidha,Bi  Minja amesema kuwa mfumuko wa Bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa Mwaka ulioishia April Mwaka huu umeongezeka hadi kufikia asilimia 4.8 kutoka asilimia 4.2 kwa Mwaka ulioishia Machi2021.

Hata hivyo amesema kuwa hali ya mfumuko wa bei kwa Nchi za Afrika Mashariki kwa Mwaka ulioishia Mwezi April Mwaka huu ikiwemo Kenya na Uganda umepungua ambapo Kenya ni asilimia 5.76 kutoka asilimia 5.9 kwa mwaka ulioishia Machi huku Uganda ukipungua kwa asilimia2.1 kutoka asilimia2.7.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Soko la Majengo Jijini Dodoma Hamisi Juma amesema kuwa upatikanaji wa bidhaa kwa wafanyabiashara umeendelea kuwa wa uhakika hivyo kupelekea baadhi ya bidhaa kuendelea kushuka bei.

Naye Mkurugenzi wa Takwimu za uchumi Ofisi ya Taifa ya Takwimu Daniel Masolwa amebainisha kuwa Tanzania ilifikia wastani wa pato la mwananchi wa Dola 1,080 na kusema kuwa inaashiria kuongezeka kwa uwezo wa wananchi kununua bidhaa na huduma na kuchochea uwekezaji zaidi na kuongeza fursa za kiuchumi Nchini.

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ni taasisi ya umma iliyoanzishwa kwa sheria ya Takwimu sura 351 kwa mujibu wa sheria hiyo NBS imepewa mamlaka ya kutoa, kusimamia na kuratibu upatikanaji na usambazaji wa Takwimu Rasmi Nchini ikiwa ni pamoja na Takwimu za mfumuko wa Bei kwa ajili ya matumizi ya serikali na wadau wa Takwimu.

Na Barnabas Kisengi.

Mei, 10. 2021

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »